ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, January 10, 2013

MAAFA ZAIDI TANA RIVER UKO KENYA MAUAJI YA KIKABILA

Watu 8 wameuawa na wengine 9 kujeruhiwa vibaya mapema leo baada ya mashambulizi mapya ya kikabila kuzuka kati ya jamii za wapokomo na waorma katika kijiji cha nduru eneo la Tana River . Ripoti kutoka eneo hilo zinasema kuwa shambulizi hilo lilitekelezwa majira ya alfajiri na zaidi ya watu 200 waliojihami kwa silaha hatari wanaodaiwa kutoka jamii ya wapokomo. Taharuki bado imetanda eneo hilo huku kukihofiwa kuwa huenda idadi ya vifo ikaongezeka namna anavyotupasha mwanahabari wetu Patrick Injendi.

No comments: