Kamanda wa Polisi mkoa wa Mara,
Absalom Mwakyoma.
|
Kamanda wa Polisi mkoani Mara, Absalom Mwakyoma, amesema kuwa tukio hilo lilitokea mnamo Desemba 30, mwaka jana, majira ya usiku katika kijiji cha Kwitete, wilayani Serengeti.
Kamanda Mwakyoma alimtaja mwanamke anayeshikiliwa kuwa ni Ghati Range (30), mkazi wa kijiji hicho na kwamba anatuhumiwa kumuua mtoto wake, Ryoba Juma (3).
Alisema mwanamke huyo alimpiga mtoto wake sehemu mbalimbali za mwili wake kwa kutumia fimbo na kisha akamchoma na chuma cha moto kichwani na mikoani, baada ya mtoto huyo kukomba mboga chunguni na kuchezea kinyesi.
“Alimpiga kwa kutumia fimbo na akamchoma na chuma cha moto kichwani na mikononi na kisha akamfungia ndani kwa zaidi ya wiki moja bila matibabu, eti kwa kosa la kukomba mboga na kuchezea kinyesi,” alisema.
Alisema baada ya kumpa adhabu hiyo alimfungia ndani ya nyumba kwa zaidi ya wiki moja bila ya kumpatia matibabu yoyote hali iliyopelekea mtoto huyo kupoteza maisha na kwamba mwanamke huyo atafikishwa mahakamani wakati wowote kujibu tuhuma za mauaji.
Alisema kuwa baada ya mtoto huyo kuwa amefariki mwanamke huyo alianza kuangua kilio hali iliyopelekea majirani kufika katika eneo la tukio na ndipo mwanamke huyo akakiri kwamba alimpatia adhabu hiyo.
CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment