ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, January 19, 2013

Mfuko wa Rais wahujumiwa, zaidi ya milioni 28/- zachotwa na wanjanja

Wajanja wachache wamechota milioni 43.9 kutoka Mfuko wa Rais na wa Uwezeshaji Wajasiriamali Wadogo (SELF) zilizokusudiwa kupewa wanachama wa  Saccos ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam.

Kati ya fedha zilizochotwa Sh milioni 28.9 zimetoka Mfuko wa Rais  na Sh milioni 15 kutoka SELF zinazodaiwa kuchukuliwa na wajanja wachache wakati wanachama wa Saccos hiyo hawakuzipata.

Taarifa za ndani ambazo NIPASHE Jumamosi imezipata ni kwamba ilidaiwa katika fedha za Mfuko wa Rais wajanja hao walishirikiana na viongozi wa Mfuko huo.
Fedha hizo zilipitia katika benki ya NMB tawi la Msasani na wajanja hao walizifuatilia ili waweze kuzichukua na kuwahusisha watia sahihi ambao sio wahusika wa Saccos hiyo.

Watu hao walimtumia Ramadhani Kigonzo ambaye sasa ni marehemu na ambaye hakuwa mwanachama wa Saccos na akajifanya Mwenyekiti wa Saccos hiyo, walifanikiwa kusaini hundi ya mkopo huo.

Hata hivyo, Mwenyekiti halali wa Saccos hiyo ni  Prosper Bwemelo ambaye hakuwa na taarifa zozote juu ya ujanja huo.

Sakata hilo liliibuka baada ya Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Kinondoni , Florence Masangu, kukutana na wanachama wa jumuiya hiyo kwa ajili  kuzungumza mambo mbalimbali ya kimaendeleo pamoja na kusikiliza kero zinazowakabili.

Meya Songoro Mnyonge alikiri fedha za Saccos kuliwa lakini alisema haijajulikana ni kiasi gani kilicholiwa.

Alisema kuna fedha zilizotolewa na mfuko wa Rais kwa ajili ya kusaidia wakazi wa Mwananyamala kupata maendeleo pia zimeliwa.

Hata hivyo, alisema ameshakaa vikao kwa kushirikiana na Afisa Ushirika wa Wilaya ya Kinondoni ambapo wanaanda mapendekezo kwa ajili ya kuitisha mkutano mkuu wa Saccos ili wajadiliane kwa pamoja.

Hata hivyo, Gazeti hili lilifanikiwa kumpata Mwenyekiti wa Saccos hiyo, Bwemelo ili azungumzie sakata hilo la kuliwa kwa fedha hizo ambapo alieleza kuwa ni kweli kuna watu wachache wamezichukua hela hizo kwa njia ambazo sio za kihalali.

Alisema milioni 15/- ambazo waliingia makubaliano na mfuko wa SELF nazo ziliingia katika mikono ya watu binafsi bila Saccos kuwa na taarifa.

Bwemelo alisema awali waliingia makubaliano na Mfuko wa SELF kuhusu mkopo huo  ambapo Meneja wa Saccos hiyo Ngeza Murshid alipeleka barua ya kuomba fedha za mkopo, katika kutia sahihi wakati wa kuchukua fedha hizo aliwachukua watu wake ambao sio wahusika wa saccos. Hata hivyo, Gazeti hili lilifanikiwa kumpata Mwenyekiti wa Saccos hiyo, Bwemelo ili azungumzie sakata hilo la kuliwa kwa fedha hizo ambapo alieleza kuwa ni kweli kuna watu wachache wamezichukua hela hizo kwa njia ambazo sio za kihalali.

Alisema milion 15/- ambazo waliingia makubaliano na mfuko wa self nazo ziliingia katika mikono ya watu binafsi bila saccos kuwa na taarifa licha ya kwamba fedha hizo zimetolewa kwa ajili ya saccos ya mwananyamala.

Alisema saccos yake haikufanikiwa kuziona fedha hizo ambazo zimetolewa na mfuko wa rais wala zile ambazo zimetolewa na self.

Hata hivyo, alisema madeni hayo ni kwamba saccoss yake haitambui kwa kuwa fedha hizo hazikuingia kwenye mahesabu ya saccos.

Bwemelo alisema fedha hizo zimetolewa tangu mwaka 2010 ambapo alikuja kugundua kama kuna hela zimeliwa Novemba 2011 baada ya mfuko huo wa Rais kuja kufuatilia deni lao wakati wao hawajafikiwa na hizo fedha.

Alisema kuna baadhi ya watu walikuwa wamekopeshwa kiaina bila hata kuwa na uthibitisho wa mali yoyote ile.

"Hata mtu akija na photo copy yake ya hati ya nyumba anapatiwa mkopo bila kuhakiki kama  ni halali ama la,  kuna mikopo mingine imetolewa bila kufuata vigezo,” Alisema
Alisema katika deni la mfuko wa self wamemtaka  Murshid kulilipa deni hilo ambapo tayari ameshaanza kulilipa. Alisema kwa sasa anachokifanya ni kwenda kuangalia deni la mkopo huo umefikia hatua gani ili saccos yake iweze kukopa kiasi cha fedha waweze kujiendesha.

Alisema mikopo ambayo imetolewa kwa wanachama wao ni sh milioni 37.7 ambazo wamegoma kulipa mpaka sasa baada ya kusikia kuna watu wamekula fedha.

Bwemelo alisema deni ambalo wanachama wanadai ni sh milioni 17 ambazo mpaka sasa bado hawajapatiwa kutokana na changamoto hizo zilizojitokeza
CHANZO: NIPASHE

No comments: