![]() |
| Dk. Harrison Mwakyembe, |
Dk. Mwakyembe ametoa agizo hilo jana baada ya kuutembelea uwanja huo ili kujiridhisha kasi ya maendeleo ya ujenzi wake ili uweze kufunguliwa rasmi kwa ndege za kibiashara.
Muongoza Ndege Mwandamizi, John Chambo, alimweleza Waziri kuwa changamoto iliyoanza kujitokeza ni wizi wa nyaya za mawasiliano.
Alisema uongozi wa mkoa wa Mbeya unapaswa kuchukua hatua za haraka kukomesha hujuma hizo kwa kuwasaka watu wanaoiba nyaya hizo na kuwaomba wananchi wenye mapenzi mema wasaidie serikali kutoa taarifa za watu wanaofanya hujuma hizo ili hatua ziweze kuchukuliwa.
Alisema baada ya kukamilika kwa ujenzi wa uwanja huo yapo mashirika kadhaa ya ndege yameomba kuanza kuutumia yakiwamo Precison Air, Fastjet na Shirika la Ndege Tanzania na mengine na kwamba hali hiyo itatoa fursa kubwa kwa wafanyabiashara, mashirika na wananchi kuweza kuutumia uwanja huo kibiashara.
CHANZO: NIPASHE

No comments:
Post a Comment