ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, January 10, 2013

Mwisho wa kubadili leseni za udereva ni machi 31



Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi nchini, limetoa wito kwa madereva na wamiliki wa vyombo vya vya moto nchini ambao hawajabadili leseni zao, kubadili leseni hizo kabla zoezi hilo halijasitishwa.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Kamishina Msaidizi wa Polisi, Johansen Kahatamu, alisema zoezi la kubadili leseni za magari litasitishwa Machi 31, mwaka huu na kwamba halitaendeshwa tena baada ya hapo isipokuwa kwa madereva wanaomba leseni kwa mara ya kwanza.


“Baada ya muda huo zoezi la ubadilishaji leseni za aina zote halitafanyika tena, isipokuwa leseni hizo zitakuwa zinatolewa kwa madereva wanaoomba kwa mara ya kwanza tu,” alisema Kahatamu.

Alisema kwa wale watakaoshindwa kubadilisha leseni zao watachukuliwa hatua kali kwa kuzuiliwa kuendesha gari na  kufikishwa mahakamani.

Aidha, Kahatamu aliongeza kwamba mpaka sasa idadi ya leseni zilizotolewa hailingani na idadi halisi ya vyombo vya moto vilivyosajiliwa,  na  kwamba hali hiyo inaashilia kwamba bado kuna idadi kubwa ya madereva wanaoendesha magari bila kuwa na leseni halali.

Alisema takwimu zinaonyesha kwamba idadi ya vyombo vya moto vilivyosajiliwa ni zaidi ya milioni moja, lakini  hadi kufikia Desemba 31, mwaka jana zaidi ya leseni 616 ndizo zilikuwa zimetolewa kwa madereva nchi nzima na kati ya hizo zaidi ya 135 ni za kundi la daraja C na zaidi ya 480 ni za makundi mengine.
CHANZO: NIPASHE

No comments: