ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, January 5, 2013

Safari ya mwisho Sajuki yakamilika


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh. Jakaya Mrisho Kikwete akiweka udongo kwenye Kaburi la Marehemu Sadick Juma Kilowoko (SAJUKI) wakati wa Mazishi yake yaliyofanyika mchana huu kwenye Makaburi ya Kisutu,Jijini Dar es Salaam.
RAIS Jakaya Kikwet, jana aliongoza mamia ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam kwenye mazishi ya msanii wa filamu nchi Sadick Juma Kilowoko maarufu kama Sajuki.
Wakazi hao ambao kabla ya kwenda makaburi ya Kisutu ambapo ndipo alizikwa Sajuki, walimiminika nyumbani kwa marehumu Tabata Bima, huku wengi wakionekana na nyuso za uzuni.
Rasi Kiwete alifika katika mazishi hayo majira ya Saa 7:00 mchana pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali na viongozi wa Shirikisho la wasanii wa filamu nchini (TAFF).
Viongozi wengine waliofika katika mazishi hayo ni pamoja na Meya wa Ilala Jerry Slaa, Mbunge wa Kinondoni Idd Azan na viongozi wengine.
Ugonjwa wa Sajuki:
Mei 13 mwaka jana, Sajuki alienda nchini India kutibiwa baada ya kupatwa na maradhi ya tumbo na uvimbe katika ini na alianza matibabu katika Hospitali ya TMJ, Msasani, Dar es Salaam.
Katibu wa Chama cha Waongoza Filamu wa Wilaya ya Ilala, Rajabu Amiri, hivi karibuni alisema kuwa, marehemu Sajuki alikuwa akisumbuliwa na tatizo la upungufu wa damu, uti wa mgongo na kansa ya ngozi.
“Mwaka jana walipokuwa nchini India kwa jili ya matibabu aligundulika kuwa ana ugonjwa mwingine, tofauti na ule uliompeleka kufanyiwa upasuaji,” alisema Amiri.
Kwa mujibu wa mkewe Wastara Juma, alisema kuwa walipokuwa India (katika Hospitali ya Apollo), Sajuki alifanyiwa vipimo mbalimbali na uchunguzi ulibaini alikuwa na tatizo la uti wa mgongo na kansa ya ngozi mwili mzima.
Hata hivyo alikuwa hajapona sawasawa na alikuwa anajiandaa kurudi tena India kwa matibabu zaidi na hili alikiri kwenye kipindi cha ‘Mikasi’ kinachoendeshwa na Kituo cha Televisheni cha Eatv.
Katibu mtendaji wa Baraza la Sanaa Tanzania (Basata), Ghonohe Materego alisema kifo cha msanii huyo ni pigo kubwa kwenye tasnia ya filamu kwa kumpoteza msanii mahiri wa filamu
Alisema kuwa anatoa pole kwa familia ya Sajuki pamoja na wanafilamu wote nchini kwa kipindi kigumu kilicho mbele yao.

No comments: