ANGALIA LIVE NEWS

Friday, January 4, 2013

SIMBA NA TUSKER NGUVU SAWA KOMBE LA MAPINDUZI

Mwinyi Kazimoto wa Simba SC akigombea mpira na Khalid Aucho katika mchezo wa Kundi A, Kombe la Mapinduzi, usiku huu kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar. Timu hizo zilitoka 1-1.
Sunzu akimtoka Shikokoti
Wachezaji wa Simba na Tusker wakisali kwa pamoja baada ya mechi
Jonas Mkude akigombea mpira wa juu na kiungo wa Tusker, Khalid Aucho, kwa picha zaidi bofya read more. Picha kwa hisani ya (Bin Zebeiry blog)
Kipa wa Tusker, Samuel Odhiambo akiwa hewani amedaka mpira mbele ya mshambuliaji wa Simba, Haruna Moshi huku akilindwa na beki wake, Mark Odhiambo
Joseph Shikokoti wa Tusker akimiliki mpira mbele ya Felix Sunzu wa SImba
Jesse Were wa Tusker akichuana na wachezaji wa Simba SC
Shikokoti na Sunzu
Ramadhan Chombo akitoa pasi iliyounganishwa nyavuni na Haruna Moshi, ambayo ilipita katikati ya mabeki wa Tusker, 
Haruna Moshi akiwa ameruka juu baada ya kusukumwa na Shikokoti baada ya kuunganisha nyavuni pasi ya Chombo Redondo
Shikokoti na Sunzu
Boban akiugulia maumivu baada ya kufunga, huku akisaidiwa na Sunzu. Kulia ni kipa wa Tusker, Odhiambo akiwa ameduwaa baada ya kufungwa
Cheki shughuli hiyo, mambo ya Boban hayo
Kiungo Mwinyi Kazimoto akipiga mpira pembeni ya Ismail Dunga wa Tusker
Shikokoti akiupitia mpira miguuni mwa Sunzu
Haruna Chanongo akigombea mpira na kiungo wa Tusker, Justin Monda
Paul Ngalema akiwatoka wachezaji wa Tusker
Kocha Mkuu wa Simba, Mfaransa Patrick Liewig akitoa maelekezo kwa wasaidizi wake kabla ya mchezo tayari kwenda jukwaani,. Wengine kulia Kocha wa Makipa, James Kisaka, Kocha wa Mazozi ya Viungo, Jamhuri Kihwelo na Kocha Msaidizi Mganda Moses Basena
Makamu Mwenyekiti wa Simba, Geoffrey Nyange 'Kaburu' katikati akifuatilia mechi hiyo 

Mwakilishi wa Jimbo la Mwembemakumbi, Machano Othman Machano akisalimiana na mchezaji wa Simba SC, Haruna Moshi kabla ya mchezo wa Kundi A, dhidi ya Tusker ya Kenya, Kombe la Mapinduzi usiku huu kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar. Timu hizo zilitoka 1-1.

Mwakilishi wa Jimbo la Mwembemakumbi, Machano Othman Machano akisalimiana na mchezaji wa Simba SC, Haruna Chanongo kabla ya mchezo wa Kundi A, dhidi ya Tusker ya Kenya, Kombe la Mapinduzi usiku huu kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar. Timu hizo zilitoka 1-1.

Mwakilishi wa Jimbo la Mwembemakumbi, Machano Othman Machano akisalimiana na wachezaji wa Tusker, kabla ya mchezo wa Kundi A, dhidi ya Simba, Kombe la Mapinduzi usiku huu kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar. Timu hizo zilitoka 1-1.
Manahodha Shomary Kapombe wa Simba na Joseph Shikokoti wa Tusker wakiwa na marefa 
Kikosi cha Simba kilichotoa sare ya 1-1 na Tusker usiku huu Amaan


Na Mahmoud Zubeiry, Zanzibar
SIMBA SC imetoka sare ya kufunga bao 1-1 na Tusker ya Kenya katika mchezo wa Kundi A, Kombe la Mapinduzi usiku huu kwenye Uwanja wa Amaan mjini hapa.
Kwa matokeo hayo, Tusker inaendelea kuongoza Kundi A, kwa piointi zake tatu sawa na Simba, lakini mabingwa hao wa Kenya wana wastani mzuri zaidi wa mabao.
Hadi mapumziko timu hizo zilikuwa zimekwishafungana bao 1-1, Simba wakitangulia kupata bao dakika ya 18 mfungaji Haruna Moshi Shaaban, maarufu kama Boban au Balotelli wa Bongo kabla ya Tusker kusawazisha dakika ya 39, mfungaji Khalid Aucho.
Boban alifunga bao tamu sana kwa ufundi wa hali juu akiwa amedhibitiwa na beki ngongoti wa Tusker, Joseph Shikokoti na kuirukia pasi ya Ramadhan Chombo ‘Redondo’ kuitumbukiza nyavuni.
Baada ya kufunga bao hilo, Boban aliangukia mkono na kuumia, hivyo hakushangilia bao lake na moja kwa moja alianza kutibiwa na Daktari Cossmas Kapinga wa Simba.
Baada ya bao hilo, Simba iliongeza mashambulizi langoni mwa Tusker na Boban alikaribia kufunga tena dakika ya 30 kama si shuti lake kutoka nje sentimita chache.
Aucho alifunga bao lake akiunganisha krosi ya Jeremiah Bright kutoka upande wa kushoto wa Uwanja.
Baada ya hapo, timu zilianza kushambuliana kwa zamu hadi refa Ramadhani Kibo alipopuliza kipyenga cha kuhitimisha ngwe ya kwanza.
Kipindi cha pili timu zote zilirudi vizuri na kucheza kwa umakini wa hali ya juu, jambo ambalo lilisababisha dakika 90 zimalizike zikiwa zimefungana 1-1.
Katika mchezo huo, kikosi cha Simba kilikuwa; William Mweta, Miraj Adam, Paul Ngalema, Shomary Kapombe, Komabil Keita, Jonas Mkude, Haroun Athumani/MKussa Mudde75, Mwinyi Kazimoto, Felix Sunzu, Haruna Moshi na Ramadhan Chombo ‘Redondo’/Edward Christopher dk 52.
Tusker FC; Samuel Odhiambo, Luke Ochieng, Jeremiah Bright/Humphrey Okoth, Mark Odhiambo, Joseph Shikokoti, Khalid Aucho, Edwin Manono/Benson Amanda, Justin Monda, Ismail Dunga/Michael Olunga, Jesse Were na Robert Omonuk.

No comments: