ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, January 2, 2013

Waukaribisha Mwaka Mpya kwa Lowassa

“Salamu zangu za Mwaka Mpya kwa Watanzaniaa, nawaomba wapitishe uamuzi mgumu kwa kila changamoto watakazokabiliana nazo,” alisema

MAKADA kadhaa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) jana walikusanyika jimboni kwa aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa kufanya sherehe ya pamoja ya kuadhimisha Mwaka Mpya.

Habari zilizolifikia gazeti hili zimetaja makada hao kuwa pamoja na Andrew Change, Beatrice Shelukindo, Peter Serukamba na Hamis Mngeja ambaye ni Mwenyekiti wa Mkoa wa Shinyanga.

Akizungumza katika sherehe hizo, Lowassa ambaye ni Mbunge wa Monduli amewataka Watanzania kutumia Mwaka Mpya kwa kuitisha uamuzi mgumu.

Akizungumza katika Sherehe za Mwaka Mpya nyumbani kwake Monduli jana, Lowassa ambaye wafuasi wake wanamwita mzee wa uamuzi mgumu, alisema kuwa ni muhimu kwa Watanzania kuwa na uamuzi mgumu katika kila changamoto watakazokabiliana nazo.

“Salamu zangu za Mwaka Mpya kwa Watanzaniaa, nawaomba wapitishe uamuzi mgumu kwa kila changamoto watakazokabiliana nazo,” alisema.

Alisema hatua hiyo ni muhimu katika kukabiliana na umaskini na kuongeza kuwa mtu akiamua inawezekana. Lowassa katika moja ya mkutano ya Bunge aliitaka Serikali kuwa na tabia ya kupitisha uamuzi mgumu katika kuwaondolea wananchi kero na kumsimamia Rais, alisema bila kuthubutu ni vigumu kukabiliana na changamoto hizo.

Lowassa alitumia fursa hiyo kukanusha taarifa zilizozagaa mitandaoni kuwa sherehe yake hiyo ni ya kisiasa akisema:

“Wameandika katika mitandao ya kijamii kuwa kuna sherehe kubwa ya kisiasa. Mimi nawaambia waache porojo hizo. Nimekuwa nikiandaa sherehe hizo tangu mwaka 1995,wao wakitaka waige mfano huu,” alisema Lowassa.

No comments: