Sunday, February 3, 2013

AFCON 2013: AFRIKA KUSINI, CAPE VERDE ZAAGA MASHINDANO GHANA NA MALI ZIKITINGA NUSU FAINALI

Mubarak Wakaso wa Ghana (kulia) akishangilia moja ya mabao aliyoifungia timu yake wakati wa mchezo wa Robo Fainali ya michuano ya AFCON 2013 dhidi ya Cape Verde, mchezo uliopigwa katika Uwanja wa Nelson Mandela, Afrika Kusini usiku huu. Ghana wameshinda bao 2-0 na kufanikiwa kutinga Nusu Fainali ya michuano hiyo. 
Kwadwo Asamoah wa Ghana (kulia) akiwania mpira na Heldon wa Cape Verde wakati wa mechi ya Robo Fainali ya michuano ya AFCON 2013 iliyopigwa katika Uwanja wa Nelson Mandela, Afrika Kusini. Ghana wameshinda bao 2-0 na kutinga Nusu Fainali.
Wachezaji wa Mali wakishangilia ushindi wao leo baada ya kuiondoa Afrika Kusini katika michuano ya AFCON 2013 kwa jumla ya mabao 4-2 katika mchezo wa Robo Fainali uliopigwa katika Uwanja waMoses Mabhida jijini Durban Afrika Kusini. Kwa matokeo hayo Mali imetinga Nusu Fainali ya michuano hiyo.
Mchezaji wa Mali, Samba Diakite (katikati) akiwania mpira na wachezaji wa Afrika Kusini, Bernard Parker na May Mahlangu wakati wa mechi ya Robo Fainali ya michuano ya AFCON 2013 iliyomalizika kwa Mali kuibuka kidedea kwa bao 4-2 kwa mikwaju ya penati.

(PICHA ZOTE NA MTN FOOTBALL)

No comments: