Friday, February 1, 2013

ALICHOSEMA WAZIRI MKUU KUHUSU IDADI YA KAMPUNI ZENYE NIA KUWEKEZA MTWARA NA MENGINE


Hii ni wakati wa fujo za Mtwara. 
Waziri mkuu wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mizengo Pinda asema zaidi ya makampuni 51 yameonyesha nia ya kuwekeza mkoani Mtwara kutokana na gesiiliyogunduliwa hivyo ametoa wito wa wananchi wa Mtwara kudumisha amani ili kuvutia wawekezaji zaidi.
Amesema kutokana na hofu ya baadhi ya wawekezaji lipo tishio la baadhi ya wawekezaji kutaka kujitoa na makampuni mengine kusitisha mipango yao ya kuwekeza Mtwara kutokana na vurugu zilizotokea hivi karibuni.
Namkariri Waziri mkuu akisema “gesi inayozalishwa Mtwara ni gesi ambayo ni sehemu ya rasilimali ya Umma, ni gesi ambayo inapaswa kuwanufaisha watanzania wote ambapo viwanda vingi vitajengwa Mtwara pamoja na Lindi ambako nako vilevile gesi inapatikana, gesi inayotoka kwenye visima vya msimbati vinavyokadiriwa kuwa na karibu trilioni 3 mpaka 5 za gesi na ambapo sasa kiasi ambacho kinachoendelezwa ni kama milioni 260 tu kwa hiyo bado gesi ni nyingi”

Ameongeza kwamba “hiyo gesi ndio tunataka iletwe pale mjini Mtwara kiwanda cha kusafisha gesi kinajengwa Mtwara Mabinda, haya ndio yanayoleta mvuto kwa makampuni mengine kwa ajili ya kuwekeza katika viwanda vya mbolea na viwanda vingine kama hiki cha Nangote ambacho tunatarajia kianze kujengwa march 2013 kwa ajili ya uzalishaji wa saruji”

January 31 2013 bungeni, Mbunge wa Hai Freeman Mbowe katika maswali ya papo kwa papo kwa waziri mkuu aliitaka serikali kuwachukulia hatua za kisheria viongozi wote waliohusika kuchochea vurugu za wananchi Mtwara ambapo Waziri mkuu alimjibu kwa kusema hiyo ishu iko ndani ya mamlaka ya waziri mkuu na mamlaka ya Rais lakini kinachotakiwa kwa sasa ni kuimarisha amani na sio kumtafuta mchawi.

Namkariri akisema “Vyama vya siasa vimechangia sana katika kupotosha jambo hili, tatizo lililojitokeza ni kila mmoja alilichukua na kulitafsiri kutegemea na malengo ambayo anataka kuyafikia katika eneo lile, kikubwa sasa tumefika mahali pazuri… kubwa isiwe kutafutana uchawi”

No comments: