ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, February 21, 2013

DIAMOND ATIRIRIKA JUU YA SHUTUMA ZA KUTUMIA NGUVU ZA ZIADA AKA NDUMBA


Hivi karibuni, alijitokeza mganga wa kienyeji akidai kumfanyia Diamond Platnumz dawa za kienyeji za ziada ili aweze kuwa na nyota nzuri kwenye muziki na kung'ara kama alivyo sasa.
Mganga huyo alikwenda katika moja ya magazeti ya udaku ya hapa nchini na kudai, Platnumz amekuwa hapokei simu zake hasa baada ya kufanikiwa katika muziki na maisha yake kiujumla huku haikuwa hivyo kipindi cha mwanzo.
Diamond alikuwa kimya na muda mrefu na mara kwa mara amekuwa akikanusha habari hizi kuwa si za kweli na kusema hamjui mganga huyo na kuwa yeye hashiriki vitu kama hivyo.
Lakini hivi karibuni Diamond ameamua kuongea ukweli hasa pale alipofanya interview a kituo kimoja cha Redio cha hapa jijini Dar na kuzungumza almost kila kitu kuhusu suala hili.

No comments: