ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, February 21, 2013

Jaji apinga hoja ya serikali ya kutosikilizwa kesi ya Uamsho


JAJI Mkuu wa Mahakama Kuu ya Zanzibar, Abraham Mwampashi jana anaeendesha kesi ya viongozi wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (JUMIKI) amepinga hoja za upande wa mashataka za kutaka kutokusikilizwa ombi la upande wa watetezi wa washitakiwa kuhusu pingamizi ya dhamana.
Jaji Mwampashi alisema kuwa asingependa kupoteza muda kutokana na mambo ya kiufundi (technicality) na kama kuna pingamizi yoyote ni vizuri Serikali ipinge siku ambayo pingamizi hiyo itasikilizwa mahakamani.

Alieleza mahakamani hapo kwamba angependa kujua sababu za upande wa mashtaka kutoka ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka Zanzibar (DPP) kutoleta ombi lao mapema huku ikizingatiwa kuwa muda wa kesi hiyo ni mkubwa ambapo kisheria ungeanza kusikilizwa.
Alisema kuwa kutokana na kuwa kesi ya msingi ipo ni vizuri mahakama ikaendelea kusikiliza ombi hilo na wala asingependa kupoteza muda kutokana na mambo ya kiufundi huku akisisitiza kuwa ombi hilo liliombwa upande wa utetezi tokea mwaka jana.
“Kesi ya msingi bado ipo mahkamani kilichotaka kusikilizwa pale ni ombi la pingamizi nisingependa kupoteza muda kwa mambo ya kiufundi ‘tenchnicts) kwenye mambo ya kimsingi nimepokea ombi lakini sio jipya, sasa kama mna chohcote mtakisema hiyo siku”,alisema jaji huyo na kuongeza kuwa nataka kujua upande wa serikali kitu gani wanakipinga wakati hakuna kifungu cha sheria kinachozuwia.
Jaji Mwampashi alihoji ikiwa mahakama hiyo haina uwezo wa kusikiliza ni mahakama ipo yenye mamlaka ya kusikiliza ombi hilo na kujibiwa na Mwanasheria wa serikali kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka, Ramadhan Naseeb kuwa ni kweli ombi hilo limepokea tokea mwaka jana na sio jipya.
Hivyo alimtaka mwendesha mashtaka huyo kuwasilisha pingamizi hizo wakati ombi hilo litakaposikilizwa kutokana na ombi hilo sio jipya kwa upande wa serikali
“Kusikiliza ombi ni February 28 mwaka huu serikali kama mtapinga ni siku hio hiyo na kama mtaleta ombi ni siku hiyo, Nasema nisingependa kupoteza muda kwa mambo ya kiufundi na naomba niankhirishe kesi hadi siyo hiyo niliyoitaja.” Alisema jaji Mwampashi
Mapema Mwendesha Mashitaka wa Serikali Ramadhani Naseeb ameiomba mahakama kuu ya Vuga kutosikiliza ombi la pingamizi la dhamana katika kesi inayowakabili viongozi wa Jumuiya ya Uwamsho na mihadhara ya Kiislamu.
Naseeb alitoa ombi hilo baada ya upande wa utetezi kuwasilisha barua ya kuitaka Mahakama kufanya mapitio yake iliyoyatoa kuhusu pingamzi iliyowekwa na upande wa Mashtaka ya kuzuia wateja wao wasipewe dhamana ambapo Mkurugenzi wa Mashitaka Zanzibar (DPP) kwa mamlaka aliyopewa amefuta dhamana za washitakiwa hao.
Washtakiwa hao ni Sheikh Farid Hadi Ahmed (41) mkaazi wa Mbuyuni, Mselem Ali Msellem (52), mkaazi wa Kwamtipura, Mussa Juma (37), mkaazi wa Makadara, Azzan Khalid Hamdani (43), mkaazi wa Mfenesini, Suleiman Juma, mkaazi wa Makadara, Khamis Ali na Hassan Bakari (39), mkaazi wa Tomondo.
Washitakiwa wote kwa pomaja wanakabiliwa na mashtaka matatu yakiwemo Uharibifu wa mali, Kushawishi, kuchochea na kuwarubuni watu kufanya fujo, huku mshitakiwa Azan akikabiliwa na makosa manne moja likiwa la uvunjifu wa amanai.
Mpema mawakili wa upande wa utetezi wakiongozwa na Salim Towfiq, Abdallah Juma na Suleiman Salim uliwasilisha ombi la kuitaka mahakama kufanya mapitio yake ilioyatoa kuhusu pingamizi iliyowekwa na mkurugenzi wa mashitaka ya kuzuia dhama ya washitakiwa hao.
Toufik alisema kuwa ni vyema mahakama ikatumia busara ya kulisikiliza ombi hilo kwa sasa kutokana na wateja wake kuwa ndani kwa muda mrefu sasa. Washitakiwa hao wamerejeshwa rumande hadi Febuari 28 mwaka huu, kwa kusikilizwa pingamizi yao.

No comments: