MSANII wa Muziki wa Kizazi Kipya Bongo, Diamond Platinum ambaye jana alikuwa akitumbuiza mjini Kigoma katika sherehe za maadhimisho ya miaka 36 ya Chama cha Mapinduzi 'CCM', ubovu wa vyombo vya muziki vilivyokuwa vikitumika kwenye tamasha hilo vilimfanya kusimamisha shoo yake kwa muda hadi pale viliporekebishwa na kuanza kutumbuiza upya.
Awali Katibu Mwenezi wa chama hicho, Nape Nauye alimkaribisha na kumruhusu msanii Diamond alishambulie jukwaa kwa ajili ya kuwapa burudani wakazi wa Kigoma ambapo walipiga kelele za shangwe huku wakikimbilia mbele ya jukwaa kumuangalia star huyo mwenye mashabiki kibao ambao waliwapa wakati mgumu pia walinzi wa CCM waliokuwa wakiwazuia.
|
No comments:
Post a Comment