Sunday, February 3, 2013

Hati ya Muungano Tunayo – Dr.Shein

Juzi nilibahatika kuhudhuria na kusikiliza kwa makini hotuba ya ufunguzi wa sherehe za kutimiza miaka 36 ya kuzaliwa kwa CCM. Dr.Shein, rais wa Zanzibar na pia Makamo Mwenyekiti wa CCM – Zanzibar ndiye alikuwa mgeni rasmi katika sherehe hizo. Nilikwenda hapo kama ‘observer’.
Hotuba yake ilijaa vijembe, kejeli na dharau kwa wale anaowahisi yeye kuwa hawautaki Muungano wa sasa (serikali mbili –kama tulivyo).
Jambo kubwa sana alilolisma Dr.Shein ni kuwa ‘HATI YA MUUNGANO IPO ZANZIBAR’; KWA KUMNUKUU ALISEMA HIVI: “Hati ya Muungano tunayo” — Dr.Shein

Alisema Dr.Shein kuwa anashangaa sana kuona baadhi ya watu wanataka kujua ilipo hati ya Muungano lakini alisema hawajafanya juhudi za kuitafuta kwani serikali inayo na nakala yake ipo makao makuu ya Umoja wa Mataifa, New York.
“Hati ya Muungano ipo pale IKULU Zanzibar kuna chumba na meza inayotumika kuwekea saini anetaka kuiona aende Umoja wa Matifa wanayo kopi hakuna haja ya kuhangaika”, alisema Dr.Shein akinukuliwa na gazeti la kila siku la Zanzibar Leo, gazeti la serikali ya mapinduzi ya Zanzibar la tarehe 1 februari 2013
Alisema kuwa Muungano wa serikali mbili unatosha kwa Zanzibar kwani ndio pekee unaoweza kuwaletea manufaa wananchi
Alisema Tanganyika na Zanzibar zilipoamua kuungana hazikufanya hivyo kw akubahatisha kwani zilitambua umuhimu wa kuwa na muungano wa pande zote mbili
Alisema kuwa Zanzibar katika muungano huo imekuwa inafaidika kwa kiasi kikubwa kutokana na wengi wa Wazanzibari wanaishi eneo kubwa la Tanzania bara kuliko watu wa bara wanaoishi Zanzibar
“Nilipokuwa Makamu wa Rais nilitembelea mikoa mbali mbali ya Tanzania na kila nilipoenda nilikutana na Wazanzibari, tuutuzeni Muungano wetu kuona unabakia imara na lazima tutafakari ndani ya miaka hii 39″, alisema Dr.Shein akinukuliwa na gazeti hilo la serikali.
Shabash ! sasa maoni yangu:
1. Kama hati hii ya Muungano ipo pale Ikulu zanzibar, kwa tukaitafute New York
2. Kwa nini UN New York waturuhusu kuiona, Ikulu — home sweet home washindwe kutuonyesha — kwa kuzingatia kuwa hii hati ni public/umma unayo haki ya kujua?
3. Pale akina Amani Karume na marais wote waliotangulia Zanzibar, wlaikuwa hawajui hilo, na hawaijui meza hiyo iliyopo Ikulu yenye Hati Hiyo.
(Hapa nitamlaumu sana Amani Karume, kwa nini alisema yale, kudai aonyeshwe hati ilhali yeye juzi tu alikuwa pale Ikulu)
4. Inanishangaza sana kuona Rais Mstaafu anasema kuwa ‘aonyeshwe hati hati ya muungano ilhali successor wake Dr.Shein anasema ipo).
5. Sasa – niwalaumu wote Dr.Shein na Amani Karume na waliotangulia –kwa nini msitueleze bayana juu ya suala hili. Sasa, tumuamini nani: Shein au Karume na wenzake: kuwa hati haipo? hati ipo? wengine wanasema Karume Sr, hakutia saini (kitu ambacho siwezi kuamini) au ninaweza kuamini? which is which? Kwa nini mnatuweka roho juu wananchi?
6. Kwa ufupi, Rais wa Zanzibar, Dr.Shein naona anazidi kuturudisha nyuma kwa msmamo wake huu wa serikali mbili. Kwa historia yetu na uongozi ulivyo na kauli zao akina Shein, Kikwete, Warioba wa Tume ya kubadilisha katiba naona kama muungano utabaki kama ulivyo. Kikwete anaamini kuwa ‘serikali haiwezi kusikiliza wachache” (suala la Mtwara); kadhalika Shein — hizi ndio rhetoric zao/zetu za utawala.
Sifikiri kama maoni ya wananchi hasa wa Zanzibar kama yatasikilizwa.
Lakini nimuulize Dr.Shein, kwa nini haiwi tatizi mtanganyika kudai serikali tatu, au kudai Tanganyika yao, hao wan-CCM Tanganyika, ila inakuwa kosa kwa mwana-CCM zanzibar au Mzanzibari kudai serikali tatu, au Mkataba au n.k?
Tuizungumze CCM: wote ni CCM hao — lakini naona mmoja anayo haki; na mwengine hana haki. WHY?
Baadhi ya kauli za Dr.Shein — zina nia ya kufitinisha pande mbili hizi kwa mfano alipose akuwa ‘wazanzibari wanaishi eneo kubwa zaidi huko Tanzania Bara lakini Wabara ….sio wengi Zanzibar”.  Huu ni ubaguzi na nia ni kufitinisha.

No comments: