Nahodha wa zamani wa Super Eagles, Kanu Nwankwo, ataizindua hospitali ya kutibu magonjwa wa moyo yenye thamani ya Naira billioni 5, tarehe 14 mwezi March 2012, huko mjini Abuja Nigeria.
Hospitali, kwa majibu wa ripoti itatoa huduma ya magonjwa yanayohusiana na moyo kwa watoto.
Pia kumekuwepo na ripoti kwamba Raisi wa nchi hiyo, Goodluck Jonathanatawaongoza watu wengine wakubwa kwenye jamii kuizindua hospitali hiyo ya Kanu.
Inasemekana kwamba mchezaji huyo wa zamani wa Ajax na Arsenal atatoa ofa ya kutibiwa bure kwa watoto kuanzia umri wa miaka 0 mpaka 12 wenye matatizo ya moyo.
Kanu alipatwa na matatizo ya moyo wakati akitokea Inter Milan kujiunga na Arsenal miaka kadhaa iliyopita. Alianzisha Kanu Heart Foundation ambayo imesaidia kutibiwa watoto wengi wenye matatizo ya moyo nje ya nchi ya Nigeria.
No comments:
Post a Comment