Wednesday, February 27, 2013

HOTELI YA DOUBLETREE BY HILTON KUGAWA TAA 200 KILA MWEZI ZINAZOTUMIA NISHATI YA JUA

Mwl. Salome Makanza wa Shule ya msingi Oysterbay akisoma risala kwa niaba ya Mwl. Mkuu Msaidizi Janeth Mdingi ambapo ameishukuru Hoteli ya DoubleTree by Hilton kwa kubuni kampeni kama hiyo ya kugawa taa zinazotumia Nishati ya Jua kwa Wanafunzi wa Darasa la Saba ambao wanakabiliwa na Mitihani kwani zitawasaidia hata Umeme utakapokatika majumbani mwao.
Mwl. Salome Makanza akikabidhi risala yake kwa Mgeni rasmi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais – Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Mh.Dkt. Terezya Huvisa. Kulia ni Mkurugenzi wa kanda wa Hoteli ya DoubleTree by Hilton Dar es Salaam Bw. Judd Lehmann. Kuhsoto ni Kushoto ni Afisa Elimu Msaidizi wa Wilaya ya Kinondoni Faustin Kikove na Mwl.Mkuu Msaidizi wa Shule ya Msingi Oysterbay Bi. Janeth Mdingi (wa pili kushoto).
Meza Kuu katika Halfa ya Uzinduzi wa taa zinazotumia Nishati ya Jua zilizotolewa na Hoteli ya DoubleTree by Hilton ya Jijini Dar es Salaam kwa shule za msingi za Mikoa ya Dar es Salaam ambapo leo wamezindua kampeni hiyo kwa kuanzia shule ya Msingi Oysterbay jijini.
Mkurugenzi wa Kanda wa Hoteli ya DoubleTree by Hilton ya Dar es Salaam Bw. Judd Lehmann akizungumza wakati wa kuzindua kampeni ya kugawa taa zinazotumia Nishati ya Jua kwa Wanafunzi wa Shule za Msingi za Mkoa wa Dar es Salaam ambapo amesema lengo lao ni kutaka wanafunzi hao wawe na ufahamu kuhusiana na Nishati mbadala ya Umeme ambayo ni rafiki wa Mazingira.
Hivyo taa hizo zitawasaidia hata kunapokuwa hakuna Umeme wa Tanesco kujisomea majumbani bila kipangamizi.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais – Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Mh. Dkt. Terezya Huvisa akitoa hotuba kuzindua kampeni ya ugawaji taa zinazotumia Nishati ya Jua iliyobuniwa na Hoteli ya DoubleTree By Hilton jijini Dar kwa wanafunzi wa shule za msingi ambapo ameipongeza hoteli hiyo kwa kubuni mradi kama huo kwani taa hizo kwa kuwa zinatumia Nishati ya jua zitawasaidia wanafunzi kujisomea na familia zao pia kupata Mwanga kunapokuwa tatizo la kukatika kwa Umeme.
Aidha amewaasa wanafunzi hao kuzitunza taa hizo na kuzitumia kwa maelngo yaliyokusudiwa.
Baadhi ya Wanfunzi wa Darasa la Saba wa Shule ya Msingi Oysterbay wakimsikiliza mgeni rasmi.
Baadhi ya wageni waalikwa na wafanyakazi wa hoteli ya DoubleTree by Hilton ya jijini Dar wakati wa uzinduzi huo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais – Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Mh. Dk. Terezya Huvisa akiendesha maswali ya masuala ya mazingira kupima upeo wa uelewa kwa Wanafunzi wa shule ya msingi Oysterbay jijini Dar es Salaa wakati akizindua kampeni ya kugawa taa zenye kutumia Nishati ya jua kwa shule za msingi za mkoa wa Dar iliyodhaminiwa na Hotel ya Doubletree by Hilton ya jijini Dar.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais – Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Mh.Dkt. Terezya Huvisa akimtunza Mwanafunzi Neema Njau shilingi Elfu taslim baada ya kujibu vyema maswali yanahusiana na Mazingira wakati wa hafla ya uzinduzi wa taa zinazotumia Nishati ya Jua zilizogaiwa kwa wanafunzi wa Darasa la saba wa shule ya msingi Oysterbay jijini Dar.
Mgeni rasmi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais – Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Mh. Dkt. Terezya Huvisa akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa taa zinazotumia Nishati ya Jua zilizotolewa na Hotel ya Doubletree by Hitlon kwa ajili ya kugawa kwa wanafunzi wa shule tofauti za msingi mkoa wa Dar es Salaam. Wanaoshuhudia tukio hilo Mkurugenzi wa Kanda wa Hoteli ya DoubleTree by Hilton ya Dar es Salaam Bw. Judd Lehmann aliyeambatana na Meneja Mkuu wa Hoteli hiyo Bw. Sven Lippinghof (mwenye tai ya Orange) na Mkurugenzi wa Masoko Hoteli ya DoulbeTree by Hilton Florenso Kirambata (nyuma ya Waziri). Kushoto (mwenye kipaza sauti ) ni Afisa Elimu Msaidizi wa Wilaya ya Kinondoni Faustin Kikove na Mwl. Mkuu Msaidizi wa Shule ya Msingi Oysterbay Bi. Janeth Mdingi (wa tatu kushoto).
Mgeni rasmi Mh. Dkt. Terezya Huvisa akihamasisha wanafunzi kutumia vizuri taa hizo hasa nyakati za kujisomea ya kukabidhi rasmi. Mkurugenzi wa kanda wa Hoteli ya DoubleTree by Hilton Dar es Salaam Bw. Judd Lehmann (wa tatu kulia), Meneja Mkuu wa Hoteli hiyo Bw. Sven Lippinghof (wa pili kushoto) na Mkurugenzi wa Masoko Hoteli ya DoulbeTree by Hilton Florenso Kirambata (kulia) na Wa kwanza Kushoto ni Afisa Elimu Msaidizi wa Wilaya ya Kinondoni Faustin Kikove na Mwl Mkuu Msaidizi wa Shule ya Msingi Oysterbay Bi. Janeth Mdingi (wa pili kushoto).
Mgeni rasmi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais – Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Mh. Dkt. Terezya Huvisa akikabidhi rasmi taa inayotumia Nishati ya jua kwa mmoja wa wanafunzi wa shule hiyo John Maganga. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Mkurugenzi wa kanda wa Hoteli ya DoubleTree by Hilton Dar es Salaam Bw. Judd Lehmann (kulia) na Kushoto ni Afisa Elimu Msaidizi wa Wilaya ya Kinondoni Faustin Kikove na Mwl Mkuu Msaidizi wa Shule ya Msingi Oysterbay Bi. Janeth Mdingi (wa pili kushoto).
Mkurugenzi wa kanda wa Hoteli ya DoubleTree by Hilton Dar es Salaam Bw. Judd Lehmann akikabidhi moja ya taa hizo kwa mwanafunzi wa darasa la saba Rebecca Andrew.
Mkurugenzi wa Masoko Hoteli ya DoubleTree by Hilton Florenso Kirambata akifanya vivyo hivyo kwa mmoja wa wanafunzi wa shule msingi Oysterbay.
Mgeni rasmi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais – Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Mh. Dkt. Terezya Huvisa akiwa kwenye picha ya pamoja na Uongozi wa Hoteli ya DoubleTree By Hilton, Uongozi pamoja na baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Oysterbay baada ya kukabidhi taa hizo.
MC wa shughuli hiyo Taji Liundi akifurahi jambo na Meza kuu.
Mgeni rasmi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais – Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Mh. Dkt. Terezya Huvisa akiteta jambo na Mkurugenzi wa kanda wa Hoteli ya DoubleTree by Hilton Dar es Salaam Bw. Judd Lehmann wakati wa hafla hiyo. Kushoto ni Mwl. Mkuu Msaidizi wa Shule hiyo Janeth Mdingi.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Oysterbay ya Jijini Dar es Salaam wakipozi na taa zinazotumia Nishati ya jua ambazo zimetolewa na Hoteli ya DoubleTree by Hilton. Wanafunzi hao wameishukuru Hoteli hiyo na kusema taa hizo zitawasaidia kujisomea hata kipindi ambacho Umeme umekatika majumbani hivyo kuongeza uwezo wao kielimu.
Na.Mwandishi wetu

Hoteli ya DoubleTree by Hilton jijini Dar es Salaam imezindua rasmi kampeni ya matumizi ya nishati ya jua ambayo itadumu kwa muda wa miaka miwili katika shule za mkoa wa Dar es Salaam.

Katika kampeni hiyo Hoteli ya DoubleTree by Hilton itakuwa ikigawa taa 200 za mezani zenye kutumia nishati ya jua kwa wanafunzi wa darasa la saba kwa shule tofauti kila mwezi, lengo likiwa nikuwafanya wawe na ufahamu zaidi juu ya chanzo kingine cha umeme ambacho ni rafiki wa mazingira kwa kupitia mafunzo katika madarasa yao.

Akizindua rasmi kampeni hiyo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Mh. Dkt. Terezya Huvisa ameupongeza uongozi wa hoteli hiyo kwa kubuni kampeni ambayo itawasaidia wanafunzi kutambua umuhimu wa nishati ya jua na kufaidika na taa wao na familia zao.

Mh. Huvisa amegawa awamu ya kwanza ya taa 200 za mezani zinazotumia nishati ya jua kwa wanafunzi wa darasa la saba katika Shule ya msingi Oysterbay na kuwataka wazitunze na kuzitumia kujisomea.

Naye Mkuu wa hiyo amtoa shukrani kwa Hoteli ya DoubleTree by Hilton akisema kampeni hiyo inazo faida nyingi kwa upande wa afya, elimu, uchumi wa nyumbani na mazingira kwa ujumla.

No comments: