Monday, February 25, 2013

MAKUNDI YA WANAUME NA MITAZAMO YAO YA KIMAPENZI KWA WANAWAKE -5

KUNDI la pili ndilo ambalo nililichambua wiki iliyopita. Kwako wewe mwanamke ni vizuri kuwajua wanaume kwa maana wao ndiyo wanaweza kukufanya uyafurahie maisha ya kimapenzi au uyachukie.

Wiki iliyopita, nilikomea kundi la pili. Na nikaanza kubainisha bahati mbaya zinazojiri nyuma ya wanawake wanaounda kundi hilo. Kwa kifupi ni kuwa wanawake wa kundi hili hupoteza mvuto wao mapema, kwani hawataonekana wana jipya.

Kwa vile ujanja wao upo kitandani, taratibu mapenzi ya wanaume hupungua kadiri wanavyozoeana.
Mwisho humuona wa kawaida kwani hisia ni zilezile, mguso ni uleule na mapenzi ni yaleyale.
Huonekana mzigo hasa pale wanaume wao wanapokuwa wanakabiliana na matatizo ya kiuchumi.Kwa kawaida, mume anapoona mambo magumu, huhitaji mwanamke ambaye anaweza kuisoma hali na kudhibiti matumizi.

Kadhalika, mwanaume hutaka kuwa na mwanamke ambaye anaweza kumpa kazi ya kugharamia chakula na matumizi madogomadogo ya nyumbani. Inapotokea mwanamke anakuwa hawezi kuingiza chochote, humtia kasoro katika harakati za maendeleo ya kimaisha.

Tatizo lingine ni kwamba inawezekana mwanamke akawa anajishughulisha lakini kwa sababu yeye anapenda kuhudumiwa, atahakikisha kipato chake anakibania ili aweze kutumia rasilimali za mwanaume peke yake. Baadaye mwanaume anaposhtuka humuona mwanamke ni mnyonyaji.

Jambo lingine baya ni kuwa wanawake wa kundi hili ni wanyonge sana mbele ya wanaume.

Hufanya hivyo ili wasipeperushe ndege. Imani yao ni kwamba wanapokuwa wapole ndivyo huongeza mvuto kwa wanaume wao.

Kwa mantiki hiyo ni ngumu hata kutambua hisia zao, huogopa kuzionesha kwa kuhofia kuachwa.

Hali hiyo hutoa mwanya kwa wanaume wa kundi hili (hasa wale wasio waaminifu), kuanzisha uhusiano na wanawake wa pembeni. Mke akisikia taarifa za usaliti wa mumewe, huogopa hata kuuliza.

KUNDI LA TATU
Aghalabu, kundi hili huundwa zaidi na wanawake wenye umri uliopevuka. Kwao pesa ni kila kitu.

Mwanaume ajitokeze mbele yake lakini kama hana fedha, asitegemee kupata penzi lenye angalau chembechembe ya mahaba. Uzuri ni kwamba ni rahisi kuwatambua kwa maana huwa hawafichi kipaumbele chao.

Ukianza naye uhusiano wa kimapenzi leo, hazitapita wiki mbili kabla hajakuonesha kile anachokitaka.

Atakuomba fedha tu na ukimpa kwa haraka, hapo unakuwa umefungulia njia.

Iwe kwa shida ndogo au kubwa, kimbilio lake ni wewe. Atakugeuza Automated Teller Machine (ATM) mpaka utajiuliza: “Hivi kabla ya kuwa na mimi alikuwa anaishije?”

Endapo siku ya kwanza akikuomba fedha utamjibu huna, unakuwa umejiwekea doa ndani ya moyo wake.

Ataendelea kubuni vitu vya hapa na pale kusudi avune pesa kutoka kwenye mfuko wako. Hata kama hana shida hasa, husisitiza mahitaji yake mpaka umpe, vinginevyo atanuna, atasusa na kukusema vibaya.

Kwake mapenzi hayakamiliki bila mwanaume kumpa fedha.
Itaendelea wiki ijayo.
GPL

1 comment:

Anonymous said...

Umetukalia rohoni kutuchambua wanawake, wanawake, sasa tumechoka ebu tuletee makundi ya wanaume