Advertisements

Wednesday, February 27, 2013

MANENO MACHACHE YA SHAA KUHUSU UHUSIANO WAKE NA MASTER J

Shaa na Master J.

Hii interview ya Shaa kwenye Leo Tena ya Super Brand Clouds FM watu wangu wa nguvu 27 ambao wamesema ni mashabiki wa Shaa waliomba niiweke kwenye web kwa sababu walisimuliwa tu ila wanataka wamsikie Shaa mwenyewe.

Ni kuhusu alichosema kuhusu taarifa za uhusiano wake na Producer Legend Tanzania Master J, ilikua ni interview ambayo hata mimi nilienjoy kuisikiliza manake Dina Marios na Shaa na wengine waliokuwepo studio walikua wamechangamka sana alafu Shaa alijiachia vizuri pia.
Alichojibu Shaa kwenye maswali ya ndio au hapana ni hapana, akisema “Ndugu mtangazaji hapana, hatuna uhusiano wowote”
Kwenye mstari mwingine Shaa alisema mpenzi wake atatambulika baada ya wazazi wake kumfahamu na kupokea mahari, baada ya hapo sasa kadi za mwaliko ndio zitaweka ukweli ambao wengi wanataka kuujua. (Millard Ayo)

No comments: