ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, February 12, 2013

Mapokezi makubwa Nigeria leo abuja

RAIS wa Nigeria, Goodluck Jonathan leo ataongoza mapokezi yenye hadhi ya Ikulu kuwakaribisha nyumbani mabingwa wapya wa Kombe la Mataifa ya Afrika, timu ya taifa ya nchi hiyo, Green Eagles.

Eagles wametwaa taji hilo baada ya kuifunga Burkina Faso bao 1-0 katika mchezo wa fainali uliopigwa usiku wa kuamkia jana na kushuhudiwa na watazamaji 85,000.
Shujaa wa bao la Nigeria alikuwa mshambuliaji anayecheza ligi ya nyumbani na klabu ya Warri Wolves, Sunday Mba.

Kikosi hicho cha Nigeria kinatarajiwa kutua mjini Abuja kikitokea Afrika Kusini kwa ndege ya kukodi na viongozi wa Serikali ya Nigeria wanatarajiwa katika mapokezi hayo kutaja zawadi kubwa watakayopewa wachezaji baada ya kutwaa ubingwa.

Baada kutua mjini Abuja, Eagles kinatarajiwa kwenda moja kwa moja Ikulu ya Rais Jonathan watakakopata mlo wa mchana, rasmi na maalum kwa ajili yao.

Mwaka 1980 na 1994 wakati vikosi vya Nigeria vilipotwaa ubingwa wa Afrika wachezaji walipewa medali za taifa hilo ikiwa ni heshima ya juu, nyumba na fedha pia.

Kwa mujibu wa Seneta David Mark ambaye alimuwakilisha Rais wa Nigeria katika fainali hizo nchini Afrika Kusini, alisema wachezaji wa Nigeria wanatarajiwa kupewa tuzo nyingi, pia kutakuwa na ziara ya kuzungusha kombe nchini Nigeria.
Tayari wachezaji wamepewa fedha kiasi cha Dola 80,000 kwa hatua ya kutinga fainali kutoka kwa tajiri mkubwa wa Afrika, Aliko Dangote.
Mwananchi

No comments: