Friday, February 8, 2013

MILENI MAGESE AFANYA BESDEI YAKE KWENYE JIJI LISILO LALA


PICHA za tukio la ‘bethidei’ ya mwanamitindo maarufu wa Bongo ambaye pia ni Miss Tanzania 2001, Millen Magese ‘Happiness’ iliyofanyika hivi karibuni New York, Marekani, 
Kupitia mtandao wa Instagram, modo huyo ambaye makazi yake ni Afrika Kusini ‘Sauzi’, aliwashukuru wadau mbalimbali kwa kumpa sapoti ya kutosha kwenye tukio hilo ambalo lilipewa jina la Birthday to Remember With Super Modal Millen and Friends.
“Nawashukuru sana jamani, bethidei yangu ilikuwa baab’kubwa hivyo asanteni wote,” aliandika Millen mtandaoni.
Katika pati hiyo, watu walijiachia kwa misosi kiwango, vinywaji vya bei mbaya na kuserebuka muziki huku wakishindwa kuamini kama ni mrembo huyo aliyeamua kuangusha sherehe hiyo.
Chanzo:GPL

No comments: