ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, February 28, 2013

MWANZA DIGITALI RASMI IFIKAPO SAA 6 KAMILI USIKU WA LEO

Mtangazaji wa Passion Fm Philbert Kabago akizungumza katika kipindi maalum na Mkurugenzi Utangazaji wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Habbi Gunze (kushoto) pamoja na Innocent Mungi (Kulia) ambaye ni Meneja wa Mawasiliano wa mamlaka hiyo leo asubuhi wakati walipo fika kwenye kituo hicho kutoa taarifa zaidi kuhusiana na uzimwaji wa mitambo ya analogia na kuingia digitali, unaokusudiwa kufanyika leo usiku ifikapo saa 6:00. 
Kwamujibu wa Mkurugenzi wa Utangazaji wa Mamlaka ya hiyo Habbi Gunze amesema kuwa maandalizi ya kuzima mitambo ya analojia ya Utangazaji wa televisheni kwa jiji la Mwanza na vitongoji vyake, yamekamilika kwa kuwashirikisha wadau wa sekta ya utangazaji hapa Mwanza ambapo mitambo hiyo itazimwa saa 6 kamili usiku wa leo tarehe 28 Februari 2013.

Elimu kwa umma kupitia mbinu mbalimbali kuhusu mchakato wa kuhamia katika teknolojia ya mfumo wa utangazaji wa digitali imekuwa ikitolewa kwa kiwango cha kuridhisha. Matangazo ya digitali yanawafikia watu asilimia zaidi ya 22% kati ya asilimia 24% ya wanaopata matangazo ya televisheni ya analojia. 

Mtangazaji wa Passion Fm Philbert Kabago (katikati) katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Utangazaji wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Habbi Gunze (kushoto) pamoja na Innocent Mungi (Kulia) ambaye ni Meneja wa Mawasiliano wa mamlaka hiyo leo asubuhi wakati walipo fika kwenye kituo hicho kutoa taarifa zaidi kuhusiana na uzimwaji wa mitambo ya analogia na kuingia digitali, unaokusudiwa kufanyika leo usiku ifikapo saa 6:00. 
Mamlaka ya Mawasiliano imeendelea kutoa agizo kwa watoa huduma za kusambaza ving'amuzi walioko Mwanza kuhakikisha kuwa kunakuwa na stoku ya kutosha ya ving'amuzi, pia mamlaka hiyo imefanya ukaguzi katika jiji la Mwanza na kugunda kuwa kuna ving'amuzi vya kutosha huku vingine vikiwa njiani kuwasili madukani kwaajili ya kukidhi mahitaji ya wengi.

Mtangazaji wa Passion Fm Devota Soteli (katikati) katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Utangazaji wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Habbi Gunze (kushoto) pamoja na Innocent Mungi (Kulia) ambaye ni Meneja wa Mawasiliano wa mamlaka hiyo leo asubuhi wakati walipo fika kwenye kituo hicho kutoa taarifa zaidi kuhusiana na uzimwaji wa mitambo ya analogia na kuingia digitali, unaokusudiwa kufanyika leo usiku ifikapo saa 6:00.
Mamlaka hiyo imeshukuru kupata ushirikiano wa karibu kutoka kwa wadau wa sekta ya utangazaji na wananchi kwa ujumla katika kipindi cha uzimaji wa mitambo ya utangazaji wa televisheni ili kufanikisha zoezi la uzimaji wa mitambo ya utangazaji ya taknolojia ifikapo tarehe 28 Februari 2013.
(Picha kwa hisani ya GSengo Blog)

No comments: