Mwenyekiti wa Kijiji cha Lugunga kilichopo wilaya ya Mbogwe mkoa mpya wa Geita, Erasto Mathias (44) hajulikani alipo baada ya kuondoka kijijini hapo tangu Novemba mwaka jana na hakuna jitihada zozote za makusudi zilizofanywa na serikali kumtafuta.
Ofisa Mtendaji wa kijiji hicho, Andrew Anthony, amethibitisha kutoweka kwa Mwenyekiti huyo aliyechaguliwa mwaka 2008 kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), alidai kuwa amekumbana na vikwazo katika jitihada za kuweka wazi tukio hilo kutokana na uongozi wa CCM kijijini hapo kumtaka asifanye hivyo kwa sababu za kisiasa.
Hata hivyo, alisema ingawa uongozi wa CCM kijijini umemzuia asitoe taarifa kuhusu kutoweka kwa Mwenyekiti huyo, lakini yeye tayari ameandika barua kwenda kwa Mkurugenzi wa Halmashauri kumjulisha juu ya tukio hilo.
“Ni kweli Mwenyekiti wetu aliondoka tangu Novemba mwaka jana akaniambia angerudi baada ya siku tatu, lakini hadi sasa hajaonekana na uongozi wa CCM umenizuia nisiweke wazi suala hili, lakini kwa vile mimi nafuata taratibu za kiutumishi, tayari nimeshaandika barua kwenda kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya kumfahamisha,” alisema.
Taarifa zilizolifikia NIPASHE zimedai kwamba uongozi wa CCM kijijini hautaki tukio hilo liwekwe wazi kwa hofu ya kupoteza madaraka ya kuongoza kijiji, badala yake umependekeza atafutwe mtu mwingine atakayekaimu nafasi hiyo.
Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Lugunga ambao hata hivyo, hawakupenda kutaja majina yao wameliambia NIPASHE kwamba wana wasiwasi huenda Mwenyekiti wao ameuawa.
Mmoja wa wananchi hao (jina linahifadhiwa) alisema mazingira ya kuondoka kwa mwenyekiti huyo na kukosekana kwa taarifa za mahali alipo kwa zaidi ya miezi mitatu sasa zinawafanya waamini kuwa huenda amekufa au ameuawa.
Alidai kuwa kabla ya kuondoka kwake mwenyekiti huyo alisimamia zoezi la kuwatambua watu waliodaiwa kumiliki “funguo malaya”ambazo walikuwa wakizitumia nyakati za usiku kufungua maduka ya wanakijiji na kuiba mali mbalimbali.
Aliendelea kusema kwamba kutokana na wizi huo iliitishwa kura ya maoni na watu kadhaa walitajwa kujihusisha na wizi huo na waliamuliwa kukihama kijiji hicho mara moja kabla ya kuchukuliwa hatua kali zaidi.
“Baada ya watuhumiwa wa wizi kufukuzwa, mwenyekiti aliondoka kwenda katika machimbo ya Nyangalata, na tulisikia kwamba huko alikutana na mmoja wa watuhumiwa ambaye alimtishia kumuua kwa sababu eti ndiye aliyesimamia zoezi la kuwatimua, ”alisema mwananchi huyo.
Kaka mdogo wa mwenyekiti huyo, Erasto Mathias, alisema kaka yake aliondoka Oktoba mwaka jana kwenda katika machimbo ya Nyangalata na alirejea Novemba na kuondoka tena kurudi huko machimboni.
Alisema tangu alipoondoka Novemba, kaka yake hajaonekana tena na amejaribu kwenda katika machimbo ya Nyangalata kumtafuta akaambiwa huko alishaondoka na kwenda katika machimbo mengine ya Nyakagwe.
Aliongeza kwamba ni wakati mwafaka kwa serikali kuingilia kati kumtafuta mwenyekiti huyo kwa sababu licha ya kuwa ni kiongozi wa kijiji, pia ana familia ya mke na watoto watano ambao wanamtegemea.

CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment