Thursday, February 21, 2013

RAIS WA KENYA AZINDUA BARABARA YA MWAI KIBAKI JIJINI DAR ES SALAAM

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mgeni wake Rais Mwai Kibaki wa Kenya wakiongozwa na Meya wa Kinondoni Mstahiki Yusuph Mwenda kutembea hatua chache kabla ya kuzindua rasmi jina la Barabara ya Mwai Kibaki linalochukua nafasi ya jina la barabara ya Old Bagamoyo leo kwenye makutano ya barabara ya Bagamoyo na Rashid Kawawa na iliyokuwa Old Bagamoyo  Februari 21, 2013.
Rais Mwai Kibaki wa Kenya akikata utepe, akishuhudiwa na mwenyeji wake Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Waziri wa Ujenzi Dkt John Pombe Magufuli na Meya wa Kinondoni Mstahiki Yusuph Mwenda kuzindua rasmi jina la Barabara ya Mwai Kibaki linalochukua nafasi ya jina la barabara ya Old Bagamoyo  kwenye makutano ya barabara ya Bagamoyo na Rashid Kawawa na iliyokuwa Old Bagamoyo.
Bendi ya Vijana Jazz ikitumbuiza wakati wa uzinduzi rasmi jina la Barabara ya Mwai Kibaki linalochukua nafasi ya jiba la barabara ya Old Bagamoyo  kwenye makutano ya barabara ya Bagamoyo na Rashid Kawawa na iliyokuwa Old Bagamoyo leo Februari 21, 2013.
Sehemu ya barabara iliyopewa rasmi jina la Barabara ya Mwai Kibaki linalochukua nafasi ya jiba la barabara ya Old Bagamoyo kwenye makutano ya barabara ya Bagamoyo na Rashid Kawawa na iliyokuwa Old Bagamoyo leo Februari 21, 2013.
Meya wa Kinondoni Mstahiki Yusuph Mwenda akimkabidhi zawadi ya kasha la Zanzibar Rais Mwai Kibaki huku mwenyeji wake Rais Jakaya Mrisho Kikwete akishuhudia katika uzinduzi rasmi wa jina la Barabara ya Mwai Kibaki linalochukua nafasi ya jina la barabara ya Old Bagamoyo kwenye makutano ya barabara ya Bagamoyo na Rashid Kawawa na iliyokuwa Old Bagamoyo.
(PICHA NA IKULU)

No comments: