Bondia Joseph Agbeko baada ya moja ya ushindi wake |
Wawili hao wanatoka katika maskani ya Bukom iliyoko kwenye kiunga cha Lebanon jijini Accra kinachosifika kwa kutoa mabingwa wengi wa dunia. Kuingia kwa mabondia hawa wawili kwenye mpambano huo kutatoa burdani ya aina yake kwa mashabiki wa ngumi wa Ghana pamoja na nchi nyingi za Afrika ya Magharibi.
IBF inaipa pongezi sana nchi ya Ghana iliyokuwa inaitwa Pwani ya Dhahabu au Gold Coast kwa kuonyesha nia thabiti ya kuinua vipaji vya mchezo wa ngumi na kuufanya mchezo huu kurudi nyumbani. Ghana inasikfika sana kwa kuweza kutoa mabingwa wengi wa nguni wa zamani ambao walisifika sana kwa uwezo wao wa kurusha masumbi wakiwamo D.K. Poison, Marvelous Nana Yaw Konadu, Azumah Nelson, Ike "Bazooka" Quartey, Alfred "Cobra" Kotey na Joseph King Kong Agbeko ambaye anatarajia kuonyesha makeke yake siku hiyo ya tarehe 8 Machi.
ISSUED BY:
INTERNATIONAL BOXING FEDERATION AFRICA (IBF/AFRICA)
DAR-ES-SALAAM, TANZANIA
No comments:
Post a Comment