Mzee Alex Kombe Enzi ya uhai wake |
Ndugu zangu Watanzania na wengine
wote. Ni zaidi tu ya siku arobaini tangu
mzee wetu Alex Kombe atutoke kwenda kwenye mapumziko ya daima. Kwa niaba ya familia yangu, ndugu zangu na
jamaa zangu na marafiki, napenda kuchukuwa fursa hii kuwashukuru wote wale
ambao walishiriki kwa hali na mali kuomboleza, kutufariji, kuwa nasi siku zile
zote za kusubirisha mipango ya kumsafirisha marehemu na kuhakikisha Alex anasafirishwa
hadi Tanzania ambako alizikwa nyumbani kwake Kilema, Moshi. Mazishi yake yalihudhuriwa na halaiki ya watu
kutoka sehemu mbali mbali.
Familia ingependa kumshukuru kila mtu
binafsi lakini haitaweza kufanya hivyo bali shukrani kwa wote, na hasa asante
zetu kwa padre Evod Shao wa Kanisa Katoliki la St. Edwards, Baltimore; Padre Callist Nyambo wa Kanisa Katoliki la All
Saints, Florida, na Wachungaji wote wa The Way of the Cross Gospel Ministries,
College Park, Maryland kwa kumuhudumia kiroho marehemu akiwa mgonjwa na baada
ya kufariki. Shukrani maalumu ziende kwa wahudumu wote wa Kanisa Katoliki la St. Camillus, Silver Spring, Maryland; kwa Rais wa Jumuia ya Watanzania DMV bwana
Iddi Sandaly kwa msaada wake usio na kifani wa kuwezesha marehemu kusafirishwa
hadi Tanzania. Shukrani pia kwa Balozi
na maafisa wote wa Ubalozi wa Tanzania Marekani kwa misaada yao. Bila ya kuwasahau woote wale ambao walisaidia
upande wa vyakula, vinywaji na wale
waliosaidia kumhudumia wakati wa matibabu.
Mimi na familia nzima tungependa kuwakaribisha wote katika sala ya kumuombea na kumkumbuka ndugu
yetu Alex ambayo itafuatiwa na chakula
cha mchana saa 7 mchana (1:00 pm sharp)
Jumapili Februari 17 katika kanisa la:
The Way of the Cross Gospel
Ministries, 3621 Campus Drive, University of Maryland College Park, Maryland
20740.
Asante na karibuni sana,
Mrs. Mary Kombe
No comments:
Post a Comment