ANGALIA LIVE NEWS

Friday, February 22, 2013

TAMKO LA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA MKOA WA MBEYA KUHUSU UCHOCHEZI WA KIDINI

Mwenyekiti kamati ya ulinzi na usalama mkoani Mbeya, Norman Sigalla
Baadhi ya viongozi wa kamati ya ulinzi na usalama mkoani Mbeya
kwa picha zaidi bofya read more
Mwandisha wa habari Felix Mwakyembe akiuliza swali kwa kamati hiyo
Mwandishi wa habari Emmanuel Lengwa akiuliza swali kwa kamati ya ulinzai na usalama
Mmoja ya wanakamati ya ulinzi na usalama mkoani Mbeya, Kamanda Diwani akijibu baadhi ya maswali yaliyoulizwa na waandishi wa habari

TAMKO LA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA MKOA WA MBEYA KUHUSU UCHOCHEZI WA KIDINI

Kwanza kabisa tungependa kutoa pongezi kwa Viongozi na Waumini wa Dini na Madhehebu mbalimbali hapo Mkoa Mbeya kuendeleza utamaduni wetu wa kuishi na kushirikiana katika shughuli mbalimbali za kijamii. Bila kuweka hisia za udini. Tunawashukuru kwa kuendelea kuvumiliana. Pamoja na kuendelea katika hali hii, kumejitokeza viashiria mbalimbali vyenye kuonyesha dalili za kumomonyoka kwa maadili, katika Mkoa wetu.

2. Kumejitokeza baadhi ya viongozi wa dini ambao wamekuwa 
Wakuzitumia nyumba zetu takatifu za Ibada kuhubiri mambo ambayohayahusiani kabisa na mambo yanayohusu Mwenyezi Mungu na mafundisho yake, kwa kuhubiri mambo ya siasa za chuki kwa dhamira ya kupandikiza chukidhidi ya Serikali au dini na madhehebumengine. Baadhi yao wamediriki kuyasema hayo hadharani kwenye miadhara yao au mikusanyiko ya waumini wao.

Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Mbeya inaona hali hii haina 
afya njema kwa mustakabali wa amani na utulivu wa Mkoa wetu na 
Nchi kwa ujumla.
3. Pamoja na mahubiri hayo pia kumekuwepo nyaraka mbalimbali za kimaandishi za sauti katika kanda, CD zenye kuhubiri chuki, uchochezi dhidi ya dini au dhehebu lingine. Kumekuwepo na video katika kanda, CD au DVD zenye kuhubiri chuki, uchochezi, dharau na kebehi dhidi ya dini nyingine au Serikali na baadhi ya kanda hizo zimediriki kuhamasisha waumini wake vurugu na hata kuua jambo ambalo Kamti ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Mbeya inaamini hakuna dini ya aina yoyote dunianiinayohimiza waumini wote kutumia kwa jambo lolote lile.
4. Baada ya kutafakari, Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Mbeya imeamua yafuatayo:- inapiga marufuku:

(i) Kuuza, kusambaza au kuonyesha, Kanda za sauti CD za sauti, Kanda 
za Video, CD, DVD, nyaraka na maandiko yoyte yenye uchochezi wa aina yoyote ile au kukashifu dini yeyote katika Mkoa wa Mbeya.

(ii) Chombo chochote cha Habari kilichopo Mkoani Mbeya kiepuke 
kuandika makala, kunakili au kurusha hewani hotuba, mahubiri au 
kuonyesha video zenye kuchochea, kudharau, kuhubiri au kukashifu 
dini yoyote ile 

5. Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa inawaasa viongozi wa dini
Mbalimbali kutohubiri siasa kwenye majumba ya Ibada kwani kwa 
kufanya hivyo watakuwa wanakiuka sheria za nchi. Mtawagawa 
waumini wenu kwa sababu waumini wanaelewa hayo si maagizo ya 
Mungu, na hayamo kwenye vitabu vitakatifu.

6. Waandishi wa Habari epukeni kushabikia matamko ya Viongozi wa 
Dini au Siasa yenye kulenga kuleta mgawanyiko katika taifa hili kwa 
Misingi ya kidini au kisiasa kwa kisingizio cha Uhuru wa Habari, 
kumbukeni Amani Umoja na Mshikamano wa Mkoa na Taifa
utategemea mchango wenu katika kushabikia au kukemea kauli hizo
bila kujali zimetolewa na kiongozi gain.

Mwisho, Serikali itamchukulia hatua za kisheria mtu yeyote atakayekwenda kinyume na haya, bila kujali itikadi yake, dini yake au wadhifa wake. Wananchi wanaaswa kuzikabidhi nyaraka, kanda CD na DVD kwa ofisi za Serikali ngazi ya Vijiji, kata Wilaya na Mkoa au kituo chochote cha Polisi. Endapo watakabidhi kwa hiyari hawatachukuliwa hatua.

Imetolewa na:
MWENYEKITI
KAMATI YA ULINZI NA USALAMA MKOA-MBEYA

No comments: