Saturday, February 9, 2013

TUFANI YA THELUJI YATIKISA JIJI LA TORONTO, CANADA

 Mji wa Toronto ulivyokumbwa na tufani ya theluji usiku wa kuamkia Ijumaa Feb 8, 2013 na kusababisha kusitisha usafiri wa mabasi na shule kufungwa na walioweza kufika kazini waliruhusiwa mapema na kama ulikua huna ulazima wa kutoka ulishauriwa kukaa nyumbani
 Mitaa ya Toronto, Canada ilivyokua ikionekana jana baada ya tufani ya theluji kuikumba mji huo na kusitisha shughuli mbalimbali ikiwemo usafiri wa ndani na shule kufungwa.
 Wakaazi wa Toronto wakipita kwa taabu baada ya theluji kuanguka usiku wa kuamkia Ijumaa Feb 8, 2013 na kusababisha shughuli mbalimbali kusitishwa.
 Theluji inavyoonekana kwenye mitaa ya Jiji la Toronto, Canada
 Sehemu ya Daraja na waendesha vyombo vya moto wakiendesha kwa uangalifu
Jiji la Toronto, Canada likiwa limechafuka kwa theluji.
Picha na Jamal Jiddawy muakilishi wa Vijimambo Toronto, Canada

No comments: