Mbali na hayo, baadhi wamekuwa hawadumu kwenye uhusiano na kujikuta leo wako na huyu kesho na yule eti kwa sababu tu uvumilivu kimekuwa ni kitu kigumu sana kwao. Yaani hawawezi kuvumilia, wakikwazwa kidogo tu wanaomba talaka.
Ilivyo sasa, ni rahisi sana mtu kuachana na mpenzi huyu na kuhamia kwa yule akitegemea kupata kitu fulani ambacho amekuwa akikikosa kutoka kwa mpenzi wake wa zamani.
Ni vema sasa tukajiuliza nini faida ya huko kuhamahama kila kukicha? Matokeo yake ni nini? Unajijengea picha gani kwa watu wanaokuzunguka?
Ni wazi kuna wakati unatendwa na kulazimika kumuacha uliyenaye na hatimaye kumpata mwingine ambaye unahisi anaweza kuisuuza roho yako.
Ni kweli inaweza kuwa hivyo, yaani unamuacha ambaye amekuwa ni mtu wa kukuliza kila siku na kuhamia kwa mwingine ambaye anakufanya uwe na amani rohoni mwako.
Ni kweli inaweza kuwa hivyo, yaani unamuacha ambaye amekuwa ni mtu wa kukuliza kila siku na kuhamia kwa mwingine ambaye anakufanya uwe na amani rohoni mwako.
Hata hivyo, inaweza kuwa kinyume chake pia. Yaani waswahili wanasema unaweza kujikuta unaruka mkojo na kukanyaga kinyesi au unaruka majivu na kukavyaga moto.
Maana yake ni kwamba, unaweza kumuacha mtu mwenye afadhali kidogo na kuhamia kwa mwingine ambaye hafai kabisa na matokeo yake ikawa ni majuto kwako.
Kutokana na hili ndiyo maana tumekuwa tukishauriwa kuwa wavumilivu kwa wapenzi wetu. Tusiwe watu wa kuchukua uamuzi wa haraka wa kuacha eti kwa sababu tumekwazwa au kutendewa yale ambayo hatukutarajia.
Niseme tu kwamba, mpaka unafikia hatua ya kusema inatosha kwa mpenzi wako iwe ni kweli umevumilia vya kutosha na kubaini kuwa kama utaendelea kuwa naye, madhara makubwa yanaweza kukupata.
Tuachane na hulka ya kuhamahama kila wakati, tujue kwamba kubadili wapenzi kila mara inaweza kuleta tafsiri mbaya kwa jamii inayotuzunguka.
Wapo wataokuchukulia kwamba wewe ni malaya, wapo watakaodhani hujatulia lakini ni wachache sana watakaojua kwamba umemuacha uliyekuwa naye na kuhamia kwa mwingine baada ya kushindwa kuvumilia tabia zake.
Kwa maana hiyo, tuna kila sababu ya kuwa makini sana kuchagua watu sahihi ambao hawawezi kutuchafua. Kubadilibadili wapenzi ni kuchafuka na tunaweza kuepuka kuchafuka huku kwa kuingia kwenye uhusiano na watu ambao tumejiridhisha nao.
Tuache kuzoazoa wapenzi, tujue kwamba wapenzi wanaweza kutupa maisha yenye amani na furaha lakini tukiingia kwenye uhusiano na watu wasiofaa, tunaweza kujuta kwa nini tumeletwa hapa duniani.
Kwa leo naomba niishie hapo, tukutane tena wiki ijayo kwa mada nyingine.
GPL

No comments:
Post a Comment