ANGALIA LIVE NEWS

Friday, March 29, 2013

DARASA LA KISWAHILI KWA WATOTO- DMV

JUMUIYA YA WATANZANIA DMV
Uongozi wa Jumuiya ya Watanzania DMV unapenda kuwapongeza wazazi na walezi kwa kuwaandikisha watoto wao kwa wingi.

Uandikishaji wa watoto unaendelea na Darasa lilianza rasmi Jumamosi iliyopita na linaendelea Jumamosi hii. Darasa hili litafanyika kila siku ya Jumamosi kuanzia saa kumi na nusu za Jioni.(4:30PM). Anuani ya Darasani ni:
3621 Campus Drive, College Park, MD

Kwa Kujiandikisha Tunaomba utume jina Kamili la Mtoto na Mawasiliano ya Mzazi au mlezi (kipeperushi na namba ya simu), kwenda: info@watanzaniadmv.org au piga simu 240-645-2131 au 301-793-2833.

Usimkoseshe Kijana wako nafasi hii ya Kujuwa Lugha yetu ya Taifa kwa Faida yake na Ya Taifa.


Wenu
Uongozi.
Jumuiya ya Watanzania DMV
www.watanzaniadmv.org

No comments: