ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, March 20, 2013

JK aagiza wanaoghushi vyeti vya taaluma washitakiwe

Rais Jakaya Kikwete ameliagiza Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania (TNMC) kuwachukulia hatua za kisheria wanaogushi vyeti katika taaluma ili kuilindia heshima ya taaluma hiyo.
 
Alisema, wafikishwe mahakamani ili wafungwe miaka mingi na kama haitoshi, muswada ufikishwe bungeni kwa ajili ya kutunga adhabu nyingine zitakazodhibiti vitendo hivyo.
 Aliyasema hayo jana jijini Dar es salaam wakati wa Maadhimisho ya miaka 60 ya baraza hilo.
 
“Kuna malalamiko kutoka kwa wananchi kwamba kuna wale wahudumu wasiozingatia maadili, na wengine ni kweli wanafanya, baraza lihakikishe linawachukulia hatua wanaokiuka maadili ili kulinda hadhi ya taaluma,” alisema.
 
Alisema, serikali itajitahidi kupunguza changamoto zinazoikabili sekta ya afya kama uhaba wa wataalamu, vitendea kazi pamoja na kuboresha vituo vya afya kulingana na ongezeko la watu na pia kupanua fursa ya mafunzo ya uuguzi, ukunga na udaktari.
 
Rais Kikwete alisema hatua hiyo itasaidia kupunguza asilimia 49 ya akinamama wanaojifungulia kwa wakunga wa jadi tofauti na alisimia 51 ya wanajifungulia katika vituo vya afya na kuongeza kuwa serikali inakusudia kujenga hospitali maalum kwa ajili ya kutoa huduma za ukunga.
CHANZO: NIPASHE

3 comments:

Anonymous said...

Ha ha ha ha ha! Real? Ni suala la unataka tuanzie wapi labda, top to bottom or bottom top?

Anonymous said...

Kwani wadau kabla Mh rais hajatoa agizo hilo, waliokuwa wana gushi vyeti walikuwa wanafanywa nini?

Anonymous said...

Nafikiri huwa wanapewa vyeo, wakigundulika wanapelekwa kupigwa brush ya chapuchapu. Wale wasio kwenye public eye huwa ningumu kugundulika, hao wanapeta tu.