Advertisements

Sunday, March 17, 2013

Kwa hili lazima Kupaza Sauti


Na Gilbert Mashurano
Ndugu Luke, Watanzania walio wengi tunaendelea kukushukuru kwa kutunganisha na kwa kutupatia habari za nyumbani(Tanzania) na za hapa Marekani.


Leo nilisoma habari iliyokuwa imeambatana na picha za Dada yetu Agness Masogange. Napenda kumshukuru Mungu aliyempatia kipaji cha uimbaji na sura ya kupendeza na kumshukuru yeye aliyetambua kipaji hicho na kukitumia katika maisha yake. Lakini picha alizokuwa amepiga zilinifanya nijiulize maswali kidogo, hasa nikiwa Mtanzania na nikiangalia tamaduni zetu za kitanzania, nikajiuliza kama nitakuwa Baba wa huyu binti na nasoma mtandao huu nitajisikiaje au kama ni kaka, au dada au ndugu yeyote, je nitafurahia kusoma huo ukurasa au nitapita haraka haraka na kujifanya sikuona kitu.


Narudia kusema haya ni mawazo yangu kuzingatia tamaduni za kitanzania. Je kama huyu ni Mama yangu au baadae akipata watoto na wakapitia ukurasa huu watajisikiaje, au kama mke wangu au baadae akiolewa mume wake akipitia ukurasa huu anajisikiaje? Bila kwenda mbele zaidi ili kuipa uzito hoya yangu ngoja nitumie maneno ya Baba wa taifa Mwl. Julius K. Nyerere, ambayo yapo kwa kingereza, nanukuu, "Of all the crimes of colonialism there is none worse than the attempt to make us believe that we had no indigenous culture of our own, or that what we did have was worthless or something of which we should be ashamed, instead of being a source of pride"

Najua wengi watakuja juu nakushangaa mawazo haya lakini nafikiri kuna ukweli katika maneno ya Rais wetu wa kwanza. Kwa picha alizozitoa Dada yetu Agness Masogange kwa Utamaduni wa Magharibi ni sawa tu na hakuna anayeweza kuhoji kitu lakini kwa utamaduni wa Kitanzania lazima kuwepo na harama ya kuuliza la sivyo tusema siku hizi wote tunafuata utamaduni wa Magharibi.

Kwa uelewa wangu kuhusu utamaduni wa Kitanzania kitu chema akiishii kwa mtu mwenyewe bali wema au uzuri wa kitu unapata maana zaidi katika jamii ya mtu anapoishi, wakati utamaduni wa Magharibu haijalishi kama uzuri au wema umetafisiliwaje na jamii, kwani kwa Magharibi uzuri uko kwenye mafanikio ya mtu binafsi, uzuri kwa hawa ndugu zetu ni ule unakufanya uwe maarufu na kupata pesa zaidi. Kwa mtanzania ni tofauti kabisa, upati heshima kwa sababu una pesa nyingi au kwa sababu ni maarufu, unapata heshima kwa mwonekano wako na mchango wako katika jamii husika.

Ni wazi tamaduni zote ubadilika kwa kuchota uzuri kutoka katika tamaduni nyingine, lakini swali ni, kila wakati sisi ndio wachotaji na wao je? Ni wakati ambao inabidi kusukuma hakiri zetu kufikiria zaidi ya hapa tulipo, na kuona mbele kwamba endapo tutaendelea kuchota uhu utamaduni bila kuchuja kwa makini kuna siku tutajikuta si Watanzania tena na tumeishakuwa kitu kingine kabisa.
Katika historia ya dunia hakuna nchi iliyojiendeleza huku ikitupa nje utamaduni wake katika hayo maendeleo, chukua mfano wa nchi kama Brazil-Samba linachezwa kila kukicha, lakini angalia sasa kila mtua anapenda kwenda huko, nenda China, Russia, Indonessia na nchi nyingi nyinginezo.
Ni jukumu la nani sasa kutunza utamaduni wa Mtanzania? Ni jukumu letu sote wenye mapenzi mema na nchi yetu, na zaidi wale ambao wanaona maana kuuenzi utanzania. Wenye watoto hapa Marekani wafundisheni watoto utamaduni wa kitanzania, tukianza na lugha, mahusiano kati ya mdogo na mkubwa, na mambo kama hayo. Tuache kuona haya kusema kwamba hili kwa Tanzania sio, na hili ndilo.

Ndugu zangu sisi ni Watanzania hata siku moja hatutakuwa Wamarekani, au Waingereza, au Wajerumani, lazima tujisikie fahari kuwa Watanzania.
Nawatakia Shughuli Njema, Asanteni

13 comments:

Anonymous said...

Mheshimiwa kwanza kabisa nashukuru kwa maoni yako, pamoja muda wako mwingi uliotumia ili kutuelimisaha wasomaji. Napenda tu kukumbusha kuwa sijawahi kusikia hata siku moja watanzania tulikaa kikao cha nchi nzima na kukubaliana kuwa a,b,na c ndiyo utamadunu wetu. Nina maana kuwa hakuna utamaduni wa mtanzania, ila Tanzania ina makabila zaidi ya 150 na kila moja lina utamaduni wake. Neno Tanganyika lilikuja baada ya wakoloni kukaa katika kikao cha Berlin 1884-85 na kuligawa bara la Afrika bila kushirikisha makabila ya Afrika. Huyu binti anaelewa kuwa Tanzania ilipata uhuru miaka 51 iliyopita, kwahiyo she is exercising her constitutional right. Inawezekana kuwa amekukera kwa mapozi yake. Naomba tu uelewe kuwa your personal opinion does not reflect Tanzanins life style, but it may dictate your doughters' life style. Kama ungetumia muda wako kufanya utafiti jinsi ya kusafirisha mahindi kutoka Rukwa kwenda Dodoma kipindi cha mvua, inawezekana ungeisaidia serikali yetu kuondokana na tatizo la njaa. I respect your intelligence, and that is why I challenge you, ni lini watz tulikubaliana kuwa pozi za namna fulani katika picha kwa mwanamke ndiyo utamaduni wetu??? Kama unaona picha za huyu dada zimekukera, nenda kasome blog zingine kama vile Mjengwa, Mbeya yetu, Shafi Dauda, Millard ayo nk. Kosoa mabinti zako na siyo watoto wa wazazi aenzako.

Anonymous said...

Hili SONONEKO lako ni very unfortunate! Mama muhusika endelea hivyohivyo, ku explore vipaji vyako mbalimbali. Hizo zote sanaa tu.

Anonymous said...

Acha zako.
Tamaduni za kiTanzania ndiyo zipi??
Kule Tanzania kuna unafiki, na uzandiki wa hali ya juu.
Kwanza asili yetu WaTanzania ni ipi??
Miaka 150 iliyopita tulikuwa tukitembea nusu uchu. wenye uwezo walivaa kajingozi kuficha mbeleni tu.
Ukitaka kujua namna tulivyo kuwa tukivaa nenda kule kalahari afrika kusini uone Bushmen wanavyovaa.

Nguo tumeletewa kwanza na Waarabu halafu wazungu.
Utamaduni huu wa kuvaa nguo ni mgeni kwetu na sikweli kwamba,nguo ni utamaduni na asili yetu Nguo ni utamaduni mgeni wa kuletwa na wakuja.

Mwaka 1870 hakuna Mtanzania alikuwa akivaa nguoz za kufunika mwili wake 90%, maximum ilikuwani 10% just kuficha mbeleni.

Unafiki urimbukeni umbumbumbu wa kutojua historia yetu halisi ndiyo unatufanya tudhani huyu dada anatembeauchi.

Waliotufundisha kuuvaa nguo wanakwenda nusu uchu,sisi tuliofundishwa kuvaa ndo tunajifanya eti tuna jua kujifunika vizuri na tunajua uchi unaanzia wapi na kuishia wapi.

Paja na Tako kwetu ni kitu kimoja, hata kwapa kwetu ni sehemu ya uchi

Anonymous said...

kaka yangu nakupa big up kwa kuchambua hii habari kwa umakini bila kificho, hili swala la vijana wa kibongo kupiga picha za kuacha maungo wazi linazidi kuota mizizi kwa vijana wa kiume na wa kike kwa upande wangu ni USHAMBA WA KUIGA UJINGA mimi nilishawahi kuishi ughaibuni na niligundua hata kwa wazungu ukikuta vijana wao wanapiga mapicha uchi au kuvaa nguo za kuacha private part nje ni zile familia zilishindikana unazikuta ni wale wa trailer park ambao wenyewe wanawaita white trash kwa mtoto wa kizungu aliyelelewa na wazazi waliostarabika anajiheshimu kwa mavazi na tabia na hata akivaa short anavaa sio hiyo ya Agnes nisimalize kurasa kusema Agnes acha ushamba dada unachofanya sio uzungu ni ushanba wa kuiga white trash au gheto

Anonymous said...

wabongo kwa kuiga inakera basi muige ya maana kama mwenzenu Wema Sepetu kafungua ofisi kajenga nyumba kanunua gari sasa wewe Agnes kuiga umeona kuacha matako nje sasa unatangaza biashara ya kujiuza mwili badilikeni mnatisha kinadada

Anonymous said...

Unaongelea utamaduni na unaleta story za baba wa taifa? Nchi ya tanzania ya wakati wa nyerere si tanzania ya leo kaka hatuko taliban we are free society. Nyerere was a dictator primitive and controlling. I don't think you will like either to go go back to the days when women walk with their breast hanging like bananas. This girl is beauty and she should wear sexy close fit her body. Mbona wewe huvai kaunda suit au mao style? Stop being ignorant let people choose what they want to wear.

Anonymous said...

Kaka hapo np na ww na nakuunga mkono na haya uliyoyaandika kwa kweli baadhi yetu ss wasichana/wanawake wa kibongo tunajidhalilisha sana kwa kuona tukipiga picha za utupu au kuonyesha baadhi ya maungo yetu ndiyo ujanja/uzungu au tupo juu.Nduguzangu wanawake tukue tuache tuache ushamba wetu wa kujitia tumekuwa na utamaduni wa nchi za wageni.

Anonymous said...

Wanaopinga hii hoja naona nyote hamna akili Kwani mnatete ujinga. Kama huna la kusema you simply shut up. Kwa wake watanzania wasiojua kuwa tuna tamaduni zetu Wala sjui wanaishi karne gani? Hadi Leo hujui ni Wtz tuna tamaduni? Eti mmesoma au mmepata walau exposure but, you still think so primitively. Nikipi unachokisifia kwa hizo picha?
Nafikiri pia mkuu Luke, you need to edit some posting. Sio kila mwenye kuona kuwa kapiga picha ailete kwako hata Kama sio njema, wanaweza kuweka Kwenye Facebook etc.

Anonymous said...

Debate ya watu wastaarabu hushindana kwa ku-reason. Unaweza kuteatea hoja yako with civility bila matusi. Hicho ndicho kipimo cha elimu. Ukiona mtu anaacha kutetea hoja yake na kuanza matusi ujue uwezo wake wa ku-reason ni mdogo, kitu ambacho ni cha kawaida kwa mstaarabu kukubali. Maswali kwa anonymous wa Marc 17, 2013 @ 11.09am ni kuwa; utamaduni wa mtanzania ni nini? Ulianza lini? Ulianzishwa na nani? Mtz anapotaka kupiga picha kulingana na utamaduni wake anatakiwa kupozi vipi? Kwa nini unapenda kufuatilia mambo yasiyo kuhusu? Huyu binti anakutegemea kwa chochote katika masha yake? Je, kila anayetofautina wewe hana akili? Kama wewe unakili, ni kitu gani cha maana ulichokifanya hapa dunia kiasi kwamba hata ukifa (God forbid) kitabaki kama kumbukumbu ya watu kujifuza kutoka kwako? Tupingane bila kutukanana kwa lengo la kuelimishana bila kijenga uadui. Anaye tofautiana na wewe siyo lazima awe adui yako. Mtazamo huo ndiyo unaaofanya mataifa yaliyoendelea yaweze kufika hapo yalipo. Kama watz tukifuata mfano huo tutafika mbali kimaendeleo.

Anonymous said...

This is none of your business, article writer. In any free society, people have the right to do anything that does not break the law. However, your opinion could work very well in Taliban Afghanistan. Good try boy.

Anonymous said...

Wee Anonymous hapo juu, ebu acha kutaka kum-infect Web Adminstrator na Ignorance ya Censorship! Moja ya chachu za maendeleo ni FREEDOMS, ikiwamo ya EXPRESSION. So acha kabisa ku contaminate hii sebule na hiyo nonsense!!

Shija Shekilango said...

kwani amevunja sheria gani!? acheni mambo ya kizamani shida za kushupalia tena muhimu zaidi kwa nchi mbona zipo nyingi sana!? stop being narrow minded dunia inabadilika

Anonymous said...

Kila mtu katika nchi yetu ana haki ya kufanya anachoona katika mwili wake, HUO NDIO USTAARABU kama mtu hataki kuangalia hulazimishwi, kasome mambo mengine. Sijaona mtu analazimishwa hapa, na sioni kwanini mtu akatazwe kufanya au kuangalia anachopenda....Kwani kuna kosa gani hapo? Samahani sana ndugu zangu Tanzania siyo Pakistan ambako msichana anaweza kuuawa kwa kutaka kusoma shule, je hiyo nayo ni utamaduni wa wapakistani au ni watu wachache kama huyo mheshimiwa anayefikiri kwamba huyo dada hapo hana haki ya kupiga picha hizo? HAKUNA KITU KINACHOITWA UTAMADUNI WA MTANZANIA...kabila langu mbarbaig wamama, wake zetu na watoto wetu wa kike siyo kosa kuacha kifua wazi, sasa huyo jamaa anataka kusema ni kosa...binafsi sioni kama ni kosa. Vipi kuhusu jirani zangu wamasai kutembea mbona wanaacha upande mmoja wazi ina maana ni kosa pia? Sijaambiwa! Ndugu zangu watz tuwe secular hizi sheria sheria zinazotungwa na watu fulani fulani, zinatungwa kwa utashi wao wala hauwakilishi binadamu wote zaidi ni kwa manufaa yao.