Wanachama wa CCM DMV wakiinuka kwenye viti vyao kushangilia kwa kishindo ushindi Uncle George Sebo aliyeshinda kwenye uchaguzi wa chama hicho kwenye nafasi ya Mwenyekiti ambao alikua mgombea pekee baada ya mgombea mwingine Mrisho Mzese kujitoa na wengine watano waliokua wakingombea nafasi mbalimbali kwa sababu ya kuona haki isingetendeka kwenye uchaguzi huo wa CCM DMV. Wagombea wengine waliopita ni Yacob Kinyemi aliyeshinda ukatibu mkuu, Faraja Isingo Katibu Uchumi na Fedha, Salma Moshi nafasi ya Katibu Itikadi na Uenezi, Mama Kimolo Uenyekiti wa UWT, Aunty Grace Mgaza Mwenyekiti Wazazi na Grace Mlingi Katibu Umoja wa Vijana
Mwenyekiti aliyekua wa muda Loveness Mamuya akimkabidhi Mwenyekiti mpya Uncle George Sebo Bendera ya Chama Cha Mapinduzi
wenyekinyiki uongozi wa CCM DMV uliokua wa muda, Loveness Mamuya akimkabidhi kitabu cha Ilani ya chama mwenyekiti mpya Uncle George Sebo.
Viongozi wa CCM DMV waliochaguliwa katika picha ya pamoja
Viongozi waliochaguliwa katika picha ya pamoja na uongozi wa zamani
Viongozi waliochaguliwa katika picha ya pamoja na wanachama wa CCM DMV
Kamati ya uchaguzi ikiwa na msimamizi Afisa Ubalozi Suleiman Saleh (watatu toka kushoto)
Viongozi waliokua wa muda CCM DMV katika picha ya pamoja
Kamati ya uchaguzi ikitangaza utaratibu wa kupiga kura
kwa picha zaidi bofya read more
15 comments:
Dhulma ya hali ya juu...endeleeni kushibisha matumbo yenu, ila mujue tu yana mwisho
hongreeni sana viongozi mliochaguliwa,leo ndio demokrasia ya kweli. tume ya uchaguzi wametuonyesha jinsi ya kuendesha uchaguzi wa haki na huru. tumehakikiwa kadi zetu kwanza kwa ustaarabu wa hali ya juu,tukapewa mmaelezo na taratibu nzuri sana ya kufuata jinsi ya kupiga kura,haijawahi kutokea utaratibu mzuri kama huo wa uendeshaji kupiga kura. halafu yule kaka aliyekuwa akizungumza kwa niaba ya tume kwa kweli anaijua kazi yake. nafikiri kuna umuhimuj makao makuu wamtumie katika kampeni zao. kwa kweli tume mmetuwekea historia katika vitabu vya siasa,kazi nzuri sana.
mbona wale walijitoa hawapo hapo? au ndio mambo ya kupiga kishabiki?kama unakipenda chama ungekuja kupiga sio kususa,si mlikuwa mnasema eti mnaipenda ccm!!!! sasa mbona hamkuja kupiga kura kama kweli mnaijua demokrasia? acheni fitina na undumiwakuwili,nyiynyi sio ccm wa kweli mlikuwa mamluki,tume imeweza kuwadhibiti sasa mmekimbia chama. nendeni vyama vingine labda ndio wataendekeza huo ujinga.chama sio fulani,chama ni wanachama hai na sio wapiga kura wenu ambao mlijidanganya mkifiri mngepewa kadi.basi sasa walete hao wanachama wenu tayari tuna viongozi tujenge chama.
yaaani CCM ni mfano wa kuigwa na watanzania woooote.yaaani ni ustaarabu na utulivu katika mambo yao,wala hamna ugomvi wala kelele.DULLAHYOO WASHINGTON DC.
HONGERAA KWA viongozi wapya wa CCM na kwa utaratibu mzuri sana na wakuigwa wa uchaguzi kwani uchaguzi unaonekana ulikuwa na utulivu na haki. KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI.
we mdau wa kwanza hapo juu..hasira za nini??kama huwezi kufurahia na kupongeza susia kama wale wenzio watano
hii ndio demokrasia inavyotakiwa. hata kama tupo kumi tutajiendeleza na kukitangaza chama.Bora hao mamluki walivyosusa maana sio wanachama wa dhati..zidumu fikra za mwenyekiti
CCM OYE!! NDUGU ZANGU WANA DMV, PAMOJA NA KUWA NIKO TANZANIA KWA MAANA SIKUWEZA SHIRIKI KATIKA MCHAKATO MZIMA WA UCHAGUZI HUU, NACHUUWA NAFASI HII KUWAPONGEZA NYOTE MLIOSHIRIKI NA WALE AMBAO WA SABABU ZAO HAWAKUSHIRIKI, KATIA UCHAGUZI HUU WA VIONGOZI WA TAWI BAADA YA TAWI KUONGOZWA NA UONGOZI WA AWALI. NACHUKUWA NAFASI HII KUUPONGEZA UONGOZI MPYA AMBAO UMECHAGULIWA KIDEMOKRASIA NA KATIKA UTULIVU NA MSHIKAMANO. NAWAPONGEZA VIONGOZI WA AWAMU YA UANZISHAJI WA TAWI CHINI YA UENYEKITI WA BI. LOVENESS MAMUYA, NA WOTE WALIOHUSIKA KATIKA KILA NAMNA KATIKA KUFANIKISHA UCHAGUZI KUENDA VIZURI NA KUPATA VIONGOZI.NI SIFA YA DMV, SIFA TA CCM, NA SIFA YA TAIFA LETU. MUNGU IBARIKI DMV, MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU IBARIKI AMERIKA. MLEZI WA TAWI.
Can a USA citizen be a member of CCM? I hope wenye mikoba hapo mnajijua.
Kwanza kuna wengine wapo humo hawajulikani wadhifa wao,au ndio wabeba mikoba na kufuata mkumbo tu?
jamani acheni ujinga,viongozi wote saba wanajua nyadhifa zao na wamegombea na wamechaguliwa.kama mna hasira sana si muende vyama vingine au fungueni shina lenu hapa mjini. maneno mengi hamjui hata mnachokizungumza,sasa aibu na sura zinawashuka. uchaguzi umefanyika na viongozi tunao,eti mwasusa!!! wenzio twala,kalagha bhao mwinyii.
hongereni mliochaguliwa huu ni ushindi wa kishindo kuchaguliwa kwa asilimia mia moja au asilimia 97 hongereni hongereni sana.
viongozi waliochaguliwa ni sita na wagombea waliojitoa ni sita, wapiga kura wote wakiwemo wagombea ni 33, nasisi wana CCM tulipolianzisha tawi tu tulianzia na wana chama 250 na mwenyekiti taifa analijua hilo na baadae wanachama wengi tu walijiunga zaida ya wale waliojiandikisha mwanzo, kama mwenyekiti aliepita alivyosisitiza umoja na mshikamano, kuna sura inaonyesha mshikamano haukuwepo, 1) nusu ya wagombea kujiondoa katika uchaguzi.
2) wapiga kura hata wale wa mwanzo kabisa hawakufika ha robo ya walioshiriki kupiga kura, inaonekana kuna mpasuko mkubwa hapo ndani ya CCM na ni aibu hata kumpelekea mwenyekiti wa taifa kuona huu mchakato wa kupiga kura, inaonekana kundi lililojiengua linakubalika na wanachama wengi na ndio wengi nao hawakushiriki, idadi ya wanachama wa CCM ni wengi mno na inatisha vipi wapigakura wanakuwa ndio wale wale tuliowazoeya hatuoni sura mpya, nina mashaka na hata ile idadi tuliokuwa nayo walituficha kutueleza ukweli.
Je tutafika?
na mimi nitanunua nyumba mwakani nigombee
The good thin about speaking the the THRUTH , you don't have to remember what you said before ..... Tuliambiwa wanachama tuko 250. Na nusu yetu pale kwenye mkutano mkuu ilikuwa Mara yetu ya kwanza kushiriki Kwani tulipigiwa simu ( jina mfukoni) tuje kumpigia Kura Mzee George , sasa pale tulikuwa 33 tuu Pamoja na hao wagombea. Sasa hao wanachama wengine 217 walikuwa wapi... Nahizi habari hata mwenyeti wa Taifa anazo.... Katibu wa tawi ukiuliza hivi sasa wana chama wako wapi utajibu nini... ? "Before you are a leader, success is all about growing yourself. When you become a leader, success is all about growing others." Sasa sisi tunajifunza nini kwenu , may be disfuntional family & lies . Yah should be ashamed of your self . DMV mkazi & mkereketwa wa tawi .
mimi kama mwana ccm nimechukizwa sana na mwenyekiti wa kwanza kijitoa ni mapema sana kwa tawi ambalo ni changa pili unapoanzisha kitu lazima ukae kwa mda before uondoke ili kuepusha matatizo wengi mnafaamu ccm kila mtu kaichoka lakini kwa nguvu na ushabiki ni wengi walijiunga kama mlivyoona siku ya ufunguzi sasa basi baada ya mwenyekiti kufanya kazi yote ya kuturudisha ccm leo gafla anajitoa hii ni kwamba kaona ccm inakasoro au kuna matatizo hatuyajuwi ??hili limenifanya nisisogee kabisa kwenye hili tawi juwa umeondoka na na wengi au kama ni pesa umeshapata basi angetueleza na sisi tuliyekuwa tunamfuata mdau wa ccm
Post a Comment