ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, March 20, 2013

MAKAMU WA RAIS DK GHARIB BILAL ATOA MKONO WA POLE KWA WAFIWA WA MSIBA WA WA ALIYEKUWA ASKARI WA USALAMA BARABARANI, WP ELIKIZAELI LOKISA NNKO, ALIYEFARIKI DUNIA KWA KUGONGWA NA GARI

Picha ya Marehemu enzi za uhai wake.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiweka saini katika kitabu cha maombolezo ya msiba wa aliyekuwa askari wa Usalama Barabarani, WP Elikizaeli Lokisa Nnko, aliyefariki dunia kwa kugongwa na gari na dereva ambaye hadi sasa hajajulikana wakati akiwa katika majukumu yake ya kikazi eneo la Bamaga Mwenge jijini Dar es Salaam jana.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimfariji Prince David, mtoto wa aliyekuwa askari wa Usalama Barabarani, marehemu WP Elikizaeli Lokisa Nnko, aliyefariki dunia kwa kugongwa na gari na dereva ambaye hadi sasa hajajulikana wakati akiwa katika majukumu yake ya kikazi eneo la Bamaga Mwenge jijini Dar es Salaam jana.
Kutoka (kulia) ni Mume wa Marehemu, David Erasto Luharara, watoto wa marehemu, Prince David na Abdulhaman David, wakiwa na huzuni.
Baadhi ya waombolezaji wakiwa nyumbani kwa marehemu kuomboleza msiba huo.Picha na Ofisi ya Makamu Wa Raisi

No comments: