Hili liko wazi huko mtaani tunakoishi. Wapo wake za watu ambao wamejikuta wakiaibika kwa kufumaniwa wakibanjuka na mashemeji zao. Hii imetokana kufuatia wao kujirahisi na kutoona tofauti kati ya waume zao na mashemeji.
Atakuwa anakuletea zawadi kama shemeji, anakutumia vocha kama shemeji, wakati mwingine wewe mwenyewe unamuomba na anakupa lakini kumbe mwenzako ana lake jambo, anakulainisha tu na kwamba kuna siku atakuomba penzi. Wapo ambao yamewakuta!
Wanawake wengine ambao ni wanywaji wa pombe wamekuwa wakijikuta wanaingizwa mkenge kiulaini. Shemeji yako anaweza kukuambia anataka kukuchukua kwenda kukupa ofa ya bia. Kwa kuwa mumeo hayupo na kwa uroho wako unaweza kukubali kumbe nia yake akuleweshe kisha ale ‘tunda’ la mumeo.
Achana na hilo, shemeji yako si mtu wa kumvalia kanga moja. Wapo wanawake ambao sijui wana akili za aina gani. Unaweza kumkuta kakaa sebuleni huku kavaa kanga moja, anakuja shemeji yake, anaendelea kukaa pale akiamini eti hakuna tatizo kwa kuwa ni shemeji.
Shemeji? Jamani ulimwengu wa sasa umekwisha. Wapo wake za watu wameshabakwa na mashemeji zao, wapo ambao sasa hivi wameachika kwenye ndoa zao kwa sababu ya mashemeji lakini pia kuna ambao mpaka leo hii wanatongozwa na mashemeji zao lakini wala hawasemi kwa waume zao.
Wanakaa kimya bila kujua kuwa ni hatari kubwa. Ukiona shemeji yako anakuingizia mambo ya mapenzi au anafanya mambo ambayo yanaonesha kutokukuheshimu, kwanza unatakiwa kuwa mkali kwake. Mweleze jinsi usivyofurahishwa na tabia zake lakini ukiona hakuelewi, mwambie mumeo.
Nasema hivi kwa kuwa ukimchekea bila kuonesha kukerwa na tabia zake ipo siku mumeo anaweza kubaini ukaribu wenu na kuhisi unamsaliti.
Kikubwa hapa ni kujua kwamba si kila shemeji ni wa kumchekea, wengine ni sumu ya ndoa yako kwani wanaona kaka zao wanafaidi hivyo nao wanataka kuonja wasivyostahili.
Katika hili la ushemeji, simaanishi ndugu wa mwanaume tu. Kuna wale mashemeji ambao ni marafiki wa mume wako. Yaani hawa ndiyo wa kuwa makini nao sana. Baadhi yao ni wepesi sana kukutongoza hasa kama utajionesha kuwa ni ‘maharage ya Mbeya’.
Ndiyo maana nawasihi wake za watu na wale wenye wapenzi wao kujiheshimu sana kwa wanaume wa pembeni. Huna sababu ya kujishebedua wala kujirahisi na kujilainisha kwao kwani mwishowe wanaweza kukuharibia uhusiano au ndoa yako.
Global Publishers
No comments:
Post a Comment