ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, March 20, 2013

MIMBA NI KIGEZO CHA KUOANA?-2


WAKATI mwingine usichukie wala kukunja ndita unapokutana na majaribu katika maisha yako. Matatizo ni sehemu ya maisha...ni ukomavu wa kiakili wa kuyakabili makubwa zaidi mbele ya safari yako. Jivunie majaribu na pambana nayo kwa kila hali, utashinda.Mwanasaikolojia mmoja mashuhuri nchini, aliwahi kusema ni vyema watu wakayapenda matatizo yao. Hata kama una gumu linalokushinda na kukutesa, silaha kubwa yenye nguvu ni kupenda tatizo hilo. Sema, hili ni langu - litapita!
Hapo nazungumzia katika upande wa maisha yetu ya kila siku lakini pia hata katika mapenzi, kuna wakati unaweza kukutana na mambo yakakuchanganya sana akili yako. Wanawake wanakukukataa, wanaume wanakukashifu na unajikuta mwili wako ni kama gazeti, kwa kuwa wengi wameufunua na kuusoma!
Siyo mwisho wako. Pambana, siku moja utasimama kifua mbele ukishangilia ushindi. Pamoja na yote hayo, yeyote mwenye utashi timilifu ni mkali wa kusaka maarifa. Naam! Kusoma ndipo kwenye nafasi kubwa zaidi ya kuongeza maarifa kuliko kusikia.
Wewe ni mwerevu kwa kuchagua kusoma ukurasa huu. Nakuhakikishia uamuzi wako ni sahihi kwa sababu baada ya hapa, utakuwa umeongeza kitu kikubwa sana kichwani mwako. Itakuwa bora zaidi kwa yule ambaye atakuwa amejifunza, kuhifadhi na kufanyia kazi yale ambayo ameyasoma hapa. Naendelea na mada yetu tunayojadili kuhusu suala la ujauzito. Mengi tuliona wiki iliyopita, leo tunaendelea katika hatua nyingine.

FAHAMU JAMBO HILI MUHIMU
Rafiki zangu wapendwa, kama tulivyoona katika vipengele vilivyopita kwenye toleo la wiki jana, suala la kupata mimba kabla ya ndoa (hasa kwa wale ambao hawaishi pamoja) si sahihi na ni jambo la hatari.
Kupata mimba kabla ya ndoa, hakukubaliki katika imani yoyote ya dini, bila shaka hata Wapagani hawaruhusu jambo hili. Wakati tunapoendelea kujadili kuhusu mada hii, lazima utambue kwamba utakuwa upo kwenye makosa na dhambi kwa kufanya kitu kilicho kinyume na maadili ya imani unayoabudu.
Najua wengi hawapendi kusikia jambo hili, lakini ndiyo ukweli wenyewe. Si sahihi kukutana kimwili kabla ya ndoa. Sisemi haya nikimaanisha labda mimi ni msafi sana, la hasha! Huenda nami kuna mahali niliwahi kuteleza, lakini hapa tujadili namna ya kushughulikia tatizo hili na maisha yaendelee yakiwa kwenye furaha tele. Twende tukaone zaidi...

UMEPATA MIMBA KABLA YA NDOA?
Je, wewe unayesoma hapa umepata mimba kabla ya ndoa na unahaha namna maisha yako yatakavyokuwa baada ya tukio hilo? Je, unafikiria jinsi utakavyoishi na familia yako ukiwa na ujauzito?
Ni kweli ni magumu kidogo kwa maisha ya kawaida ya kibinadamu lakini kwa kuwa memba wa All About Love, utakuwa mwenye ufahamu na utajua namna ya kukabiliana na changamoto hiyo huku maisha yako yakiendelea kuwa ya amani na furaha tele.

(i) Hatua ya kwanza
Mshirikishe mwenzako. Kama una uhakika kuwa mimba uliyonayo ni ya mhusika wako, mweleze ukweli. Tafuta muda mzuri, mwite na umjulishe juu ya ‘bahati’ mbaya iliyotokea. Hakikisha katika hatua hii, huoneshi kuwa umekutana na tatizo kubwa katika maisha yako.
Aone unazungumza juu ya ‘baraka’ ingawa imekuja kwa muda ambao si sahihi. Usioneshe matarajio yoyote katika mazungumzo yako. Kikubwa ni kumjulisha tu kuwa sasa una mimba yake!

(ii) Hatua ya pili
Katika matamshi yako usioneshe kabisa kwamba mimba hiyo ni sababu ya kukuoa na anachotakiwa kufanya ni kufunga ndoa na wewe au kuhamia kwake. Achana na vitisho kabisa.

(iii) Hatua ya tatu
Acha papara, mpe nafasi ya kuzungumza. Msikilize kwa makini maoni yake. Vyovyote itakavyokuwa, maadamu una uhakika mimba ni yake kila swali lake litakuwa na jibu. Kubaliana na mawazo yake, lakini kamwe usiruhusu mawazo yake ya kwenda kutoa mimba yakaingia kichwani mwako.

(iv) Hatua ya nne
Sasa mnatakiwa kujadiliana pamoja. Zungumza naye kuhusu athari (angalau zile za kawaida kabisa kama matatizo ya uzazi nk) za kutoa mimba. Mwache huru aamue anachotaka. Kama mnapendana na lengo lenu ni ndoa, basi hapo inaweza kuwa tiketi ya kuharakisha hilo ili kukuepusha na aibu nyumbani kwenu.
Kama atasema hayupo tayari usimng’ang’anize ila zungumza naye kuhusu utaratibu unaofaa wa kulea mimba na mtoto hapo baadaye ikiwa ni pamoja na kujitokeza nyumbani kwenu (kupitia wazee) na kueleza kuwa anahusika na mimba yako na kwamba (labda) anajipanga kwanza kabla ya kuchukua uamuzi mwingine hapo baadaye.
Mada bado inaendelea, wiki ijayo tutaingia katika hatua nyingine, USIKOSE!

Joseph Shaluwa ni Mshauri wa Mambo ya Mapenzi anayeandikia Magazeti ya Global Publishers, ameandika Vitabu vya True Love, Let’s Talk About Love na All About Love vilivyopo mitaani.

6 comments:

Anonymous said...

Samahani unaongelea kabla mimba ni bahati mbaya, Asilimia kubwa ya wanawake siku hizi hujishikisha mimba makusudi ili amtrap mwanaume. Na dhumuni kubwa ni kuolewa. Siku hizi kuna kila aina ya contaception na dunia imeelimika kama hauko tayari kushika mimba utachukua hatua zote. Ila kuna wanawake wanafanya makusudi na wanaume wa siku hizi wameshtuka utaishia kulea mimba peke yako. Ni bora ungelenga suala hilo zaidi la kujishikisha mimba ili mwanaume akae na wewe.

Anonymous said...

Ni ni lazima tujichunge na kuwa waangalifu.kuna wanawake wengine wanaakili za ajabu saaana.kamdanganya mwenzake kwanba anatumia vidonge vya uzazi kumbe wapi na alipopata mimba akaenda kuitaarifu familia yake eti kapata Mchumba.akaamua kutoa maamuzi yote kwamba ni lazima jamaa amuoe tena kwa nguvu jamaa alipisema hayupo tayari yule mwanamke akamwambia jamaa asije kumuona mtoto pesa za matumizi jamaa anatoa lakini mwanamke ametia ngumu kumruhusu baba kumuona mtoto wake. Bora tujichunge na watu wa namna hii

Anonymous said...

Je wewe ulisha kaa chini ukamuliza Huyo mwanamke story au unasikia one side?. Kuna wanaume wengine waongo wanataka kuonekana kama victim. When you climb in bed with someone there's always a chance someone will get pregnant if you are not ready for a baby use protection. Take care of your babies.!!!!

Anonymous said...

mdau wa tatu hata ukimuuliza huyo mwanamke atakupa story ya uongo ya kujifanya ni victim, Hakuna mwanamke anashika mimba bahati mbaya, huwa mnajishikisha mimba ili wanaume wawaoe halafu mukikataliwa mnaanza kusambaza uongo mji mzima,na kama ulivyosema if you are not ready use protection sasa wewe mwanamke inakuwaje na wewe ushike ina maana ulikuwa uko ready. wacheni upumbavu huo wanaume wa siku hizi haumkamati kwa kujishikisha mimba infact akisikia tu anatoka baruti. Mifano tunayo kibao hasira eti kumkomoa unampeleka child support. matokeo yake umeishia mkono mtupu na bwana hakutaki vilevile mwandishi wa hii topic naomba uandike maana itawanufaisha hawa madada zetu waache ujinga wao.

Anonymous said...

Why do you place the blame on a woman? It takes two to tangle my brother. If a man is not ready for a child use protection. As women we need to value ourselves. If a man doesn't want you keep it moving. Men come dime a dozen. When you climb in bed with someone there's always a possibility of pregnancy. Let's all be smart and protect ourselves.!!!!!!

Anonymous said...

The only victims you have in this situation are those innocent children. Let's all take time and think about that