Waandaaji wa pambano hilo Abuu chaka na Bigright Promotion wamelipeleka pambno hilo katika ukumbi wa CCM Mwinjuma kwa kuwa kuna usalama mzuri na pakingi kubwa ya magari na ukumbi huo umekarabatiwa ndani na kuwa katika hali nzuri na migahawa ya chakula na vinywaji na baa ya kisasa ipo ndani isitoshe kutakuwepo na mapambano makubwa ya utangulizi wa mabondia wazoefu na wakongwe wa ngumi kama Joseph Marwa atazipiga na Amour mzungu ,wakati ramadhan Kido akipimana ubavu Musa mbabe hawa ni mabondia wa uzito wa juu watazipiga raundi nanenane, pia husein mbonde atazipiga na mwaite juma,Martin Richard atazipiga na Faraj Sayuni, Josef piter”mbowe”(mototo wa golikipa wa zamani wa simba piter paulo) atazipiga na Zumba kukwe na mapambano mengineyo mengi ya vijana wanaochipukia kwa kasi katika fani ya masumbwi nchini ili kuviimarisha vipaji vyao kwa maandalizi ya kutoa mabingwa wengine wa baadae wa dunia, mapambano haya hayajapata mfadhili wala mdhamini kwa hiyo wanaombwa wajitokeze kuusaidia mchezo huu.
IBRAHIM ABBAS KAMWE
General secretary -Tanzania Professional Boxing Organization
No comments:
Post a Comment