Advertisements

Wednesday, March 6, 2013

MWENYEKITI WA JUKWAA LA WAHARIRI ABSALOM KIBANDA AVAMIWA NA KUJERUHIWA VIBAYA

Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri na Mhariri Mtendaji wa New Habari, Absalom Kibanda,akipata matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili baada ya kuvamiwa. (Picha na Mtandao wa Mabadiliko)
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri na Mhariri Mtendaji wa New Habari, Absalom Kibanda, amekimbizwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili baada ya kuvamiwa na kisha kujeruhiwa na watu wanaosadikiwa kuwa majambazi.
Watu hao walimvamia na kumtoa katika gari kisha wakampiga kabla ya kumtupa na kumtelekeza umbali mdogo na nyumbani kwake.Kibanda aliokotwa na majirani na kukimbizwa hospitalini Muhimbili kwa matibabu ya haraka.Pamoja na kuumizwa hivyo, hakuna kitu chochote kilichoporwa katika gari lake.
Chanzo: Jamii Forums

No comments: