ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, March 28, 2013

Pamoja We Can Re-Build Tanzania


Nafikiria kuanzisha msukumo wa kuleta curriculum mpya katika mfumo wa elimu wa Tanzania ambayo inalenga matatizo yanayoikabili Tanzania. Curriculum hiyo iwe ya kufundisha wanafunzi matatizo ya Tanzania na kujaribu kuyapatia ufumbuzi. Namna hiyo wanafunzi watajiona kuwa wamewezeshwa katika kubadili hali yao ya baadaye na mwelekeo wa taifa lao. Kwa hivi sasa hali ya baadaye ya wanafunzi, watu na Taifa lenyewe iko katika mikono ya serikali tu. Kama wanafunzi wote, ambao ni kundi kubwa Tanzania, watajifunza kuhusu matatizo yanayokabili taifa watataka kuchangia katika mabadiliko kwa sababu maisha yao ya baadaye yanategemea hali hiyo ya baadaye kwa taifa. Tunalenga wanafunzi kwa sababu ni kundi kubwa na wako tayari kujifunza mambo mapya. Toa mchango wako hapa, tushirikiane mawazo. Karibuni - Mr.Tz

Tunachojaribu kufanya ni kubadili mwelekeo wa elimu Tanzania. Tutengeneza curriculum ambayo inasaidia vijana kuwa na "critical thinking" Hii itawezesha vijana hata wakiwa bado shule wanaanza kufanya projects za kutafuta ufumbuzi wa maswala na matatizo yanayokabili taifa. Lakini yote inahitaji nguvu ya serikali kuwa na waalimu hodari, vifaa mashuleni na mambo mengine yanayomwezesha 
mwanafunzi kujifunza.

Msanii wa kizazi kipya Mr.Tz anasema: "Nobody can re-build Tanzania, other than us, the people of Tanzania. Msifungamane na upande wowote. Tukiwa pamoja as the people of Tanzania, we can, we WILL change Tanzania., for the better. Nisikilize.." - Mr.Tz

No comments: