ANGALIA LIVE NEWS

Friday, March 29, 2013

RAIS KIKWETE, ATEMBELEA ENEO LILIPOTOKEA AJALI YA KUANGUKA GHOROFA JIJINI DAR

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa mtaa wa Indira Ghandi jijini Dar es salaam leo akiwa ameongozana na mkewe Mama Salma Kikwete kujionea mwenyewe jengo lililoporomoka asubuhi saa mbili na nusu leo Machi 29, 2013 ambapo hadi Rais anafika mahali hapo saa saba kamili watu wawili wamethibitishwa kuwa wamekufa na wengine 19 kujeruhiwa, wawili wakiwa mahututi. Juhudi zinaendelea kuokoa watu wanaosadikiwa kunaswa kwenye kifusi cha jengo hilo lililokuwa limefikia ghorofa ya 15, likijengwa ubavuni mwa Msikiti wa Shia Ithnaasheri.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo toka kwa Mkuu wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam Bw. Suleiman Kova na Mkuu wa Mkoa huo Mhe saidi Meck Sadiki katika eneo la jengo lililoporomoka mtaa wa Indira Ghandi jijini Dar es salaam asubuhi saa mbili na nusu leo Machi 29, 2013 ambapo hadi Rais anafika mahali hapo saa saba kamili watu wawili wamethibitishwa kuwa wamekufa na wengine 19 kujeruhiwa, wawili wakiwa mahututi. Juhudi zinaendelea kuokoa watu wanaosadikiwa kunaswa kwenye kifusi cha jengo hilo lililokuwa limefikia ghorofa ya 15, likijengwa ubavuni mwa Msikiti wa Shia Ithnaasheri.

1 comment:

Anonymous said...

Poleni sana ndugu zangu watanzania. Mungu azilaze pema roho za marehemu wote na majeruhi wapone haraka. Ni vizuri kutembelea eneo la maafa kwa viongozi wetu. Lakini nafikiri ni vizuri zaidi kuwaachia wataalamu wa uokoaji wafanye kazi yao. Inawezekana kuna watu bado ni wazima wamefunikwa. Sidhani kama tunawatendea haki majeruhi hao kwa kusimamisha uokoaji kutokana na ziara za viongozi wa juu hasa tukizingatia kuwa every minute count for their breath.