Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi msaada wa Usafiri aina ya Bajaji Bwana Bashir Msanda ambaye ni mlemavu wakati wa mwanzo wa ziara yake ya kukagua na kufungua miradi ya maendeleo jijini Dar es Salaam leo asubuhi.Makabidhiano hayo ambayo ni utekelezaji wa ahadi ya Rais Kikwete kumsaidia mlemavu huyo ,yalifanyika katika viwanja vya Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam
|
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiweka jiwe la msingi kuzindua rasmi ujenzi wa Taasisi ya mifupa na mishipa ya fahamu katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam leo
|
Mkurugenzi wa Huduma za Maabara Bibi Charys Ugullum akimweleza Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete jinsi maabara ya ukaguzi wa dawa na vyakula inavyofanya kazi wakati Rais alipotembelea maabara ya kisasa ya TFDA iliyopo Mabibo External jijini Dar es Salaam leo mchana wakati wa siku ya kwanza ya ziara yake ya kikazi ya siku tatu mkoani Dar es Salaam
|
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,Waziri wa Elimu Dkt.Shukuru Kawambwa(kulia),Balozi wa Korea ya Kusini Mhe.Chung(wapili kulia),Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Bwana Sadik Meck Sadik(Wapili kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa VETA Injinia Zebadia Moshi(kushoto) wakikata utepe kufungua rasmi Chuo Cha TEHAMA VETA huko Kipawa jijini Dar es Salaam leo
Rais Dkt.Jakaya Mriusho Kikwete,Waziri wa Elimu dkt.Shukuru Kawambwa(kulia) na Balozi wa Korea ya Kusini Mhe.Chung na viongozi wengine wakipiga makofi wakati wa uzinduzi wa Chuo cha TEHAMA VETA Kipawa jijini Dar es Salaam leo mchana. Picha zote na Freddy Maro wa Ikulu
|
No comments:
Post a Comment