Simba ipo katika mazingira magumu ya kuingia raundi ya pili ya Ligi ya Klabu Bingwa Afrika ikitakiwa kubadili ugenini kipigo cha nyumbani cha 1-0 kuwa ushindi dhidi ya Recreativo Libolo ya Angola leo lakini ni jukumu ambalo imewahi kulimudu miaka ya nyuma. Mara mbili.
Ili kujihakikishia kusonga mbele Simba inatakiwa kupata ushindi wa tofauti ya mabao mawili.
Lakini inaweza kuingia hatua inayofuata pia kama itashinda 1-0 na ikalamba dume katika kamari ya 'matuta' baada ya dakika 90.Kwa kuangalia jinsi Libolo ilivyocheza kwenye Uwanja wa Taifa wiki mbili zilizopita, ni jukumu zito dhidi ya timu ambayo inajipanga vizuri kukabili changamoto za kimbinu dhidi yake uwanjani.
Lakini kikosi cha Simba kilichopo Angola kitakuwa kinafahamu kuwa nahodha Juma Kaseja akiwa langoni, Wekundu wa Msimbazi waliingia robo-fainali ya Ligi ya Klabu Bingwa Africa miaka 10 iliyopita timu hiyo ikipewa nafasi finyu kuliko leo.
Simba ilipoteza mechi ya kwanza 1-0 dhidi ya Zamalek kwenye Uwanja wa Uhuru lakini nayo ikaja kushinda kwa idadi hiyo ya magoli jijini Cairo, Misri.
Ushindi wa 'matuta' 3-1 ukaiwezesha kuwa timu ya pili nchini kucheza hatua ya ligi ya michuano hiyo mikubwa zaidi kwa klabu barani baada ya Yanga mwaka 1999.
Na haikuwa mara ya kwanza.
Robo karne kabla ya 2003, pengine kikosi mahiri zaidi cha Simba kilichopata kutokea katika historia ya timu hiyo, katika moja ya matokeo ya ajabu zaidi ya michuano ya Klabu Bingwa Afrika wakati huo, muujiza mwingine ulifanyika.
Simba iliyokuwa imepoteza mchezo wa kwanza 4-0 kwenye Uwanja wa Uhuru, ilikwenda Lusaka, Zambia na kuifunga Mufulira Wanderers 5-0 na mbele ya Rais wa kwanza wa taifa hilo Keneth Kaunda.
Ni wazi basi kikosi cha kocha Patrick Liewig ambacho kimeonyesha kusuasua kwenye ligi kuu ya Bara tangu kuanza kwa duru la pili na kuhitimisha kilele cha mwenendo mbovu huo kwa kufungwa na Libolo, kitaingia uwanjani leo kupigania jezi ya Simba kikijua kuwa historia ipo upande wake.
Tatizo pekee, pengine, ambao huenda likaiathiri Simba ndani ya uwanja leo ni kutosafiri kwa kiungo Haruna Moshi ambaye hupangwa kama mshambuliaji katika timu ambayo ina mchezaji mmoja tu wa mbele; mgonjwa-mgonjwa Felix Sunzu.
Sunzu acheze ama asicheze kutokana na sababu yoyote, mategemeo ya Simba kurudia historia yanaweza kuwa kwa winga machachari wa timu ya taifa, Taifa Stars, Mrisho Ngassa.
Ngassa alikuwa kivutio cha vyombo vya habari vya Angola timu hiyo ilipotua huko juzi, kwa mujibu wa kiongozi wa msafara Zakaria Hans Pope, ambavyo vilimzonga vikitaka kufanya naye mazungumzo. Pengine kutokana na kuwapeleka puta mabeki wa Libolo katika mchezo wa kwanza.
Mbali na Simba, Azam leo itakuwa ikijaribu kulinda ushindi wake wa 3-1 wa nyumbani dhidi ya Al Nasri mjini Juba, Sudan Kusini, ili kusonga mbele kwa mara ya kwanza kwenye Kombe la Shirikisho la klabu za Afrika, ikishiriki kwa mara ya kwanza pia.

CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
No comments:
Post a Comment