Mhe. Sophia Simba ( Mb) akiongoza ujumbe wa Tanzania wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 57 wa Kamisheni kuhusu Hali ya Wanawake ( CSW) mkutano huo wa wiki mbili umeanza siku ya jumatatu hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa, wengine katika picha ni Balozi Tuvako Manongi, Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Mhe. Engera Kileo Mmari Jaji wa Mahakama ya Rufa, Naibu Mwakilishi wa Kudumu, Balozi Ramadhan Mwinyi, wengine ambao wapo katika meza hiyo ya Tanzania, ni Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Bi. Kijakazi Mtengwa na Mhe. Imani Aboud Jaji wa Mahakama ya Rufaa
Na
Mwandishi Maalum
Mkutano wa 57
wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa Kuhusu
Hali ya Wanawake (CSW), umeanza siku ya
jumatatu hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa.
Mkutano
huo wa wiki mbili na ambao hufanyika kila mwaka unawakutanisha Mawaziri
wanaohusika na masuala ya wanawake na
maendeleo ya jamii kwa ujumla, wataalamu
mbalimbali vikiwamo vyama visivyo vya kiserikali kutoka duniani kote.
Ujumbe
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika
mkutano huu unaowajumuisha washiriki kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar unaongozwa na Waziri wa Maendeleo ya Jamii,
Jinsia na Watoto, Mhe. Sophia Simba ( MB).
Miongoni
mwa wajumbe wa Tanzania ni Bi Kijakazi Mtengwa, Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Bi.
Fatma Gharib Bilal, Katibu Mkuu, Wizara
ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii, Vijana,Wanawake, na Watoto,
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Majaji wa Mahakama ya Rufaa, Mhe. Engera Kileo Mmari na
Mhe. Iman Daud Aboud.
Akifungua
mkutano huu, Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Bw. Jan Eliasson amesisitiza kwa kusema, vita vya kuutokomeza ukatili dhidi ya wanaweke lazima iwe ya kufa
na kupona.
Akaeleza
kwamba ukatili dhidi ya wanawake ni
jambo linalotokea kila mahali hata
katika nchi zilizoendelea.
Akabainisha
kwamba ili kukakibiliana na ukatili dhidi ya wanawake, panahitajika mbinu mchanganyiko kuanzia serikalini kwa kutekeleza sera za
kuwawezesha waathirika wa vitendo hivyo , kuwaadhibu wahalifu
Akaeleza
pia kwamba, wanaume na watoto wa kiume
wanatakiwa kuhamasishwa kushiriki katika kupiga vita ukatili dhidi ya wanawake
ikiwa ni pamoja na kuwajengea utamaduni wa kuwajibika katika shughuli
mbalimbali za kifamilia.
Akaeleza zaidi kwamba,
vitendo hivyo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto wakike vinafanyika katika maeneo yenye vita na migogoro lakini pia
vinafanyika katika nchi zenye amani na utulivu. Na kama hiyo haitoshi
vinatendeka pia kwenye miji mikuu na
halikadhalika vijijini.
“Ni vitendo”
anasema Naibu Katibu Mkuu. “Vinavyotokea katika maeneo ya wazi na yaliyojificha
pia. Na kwa kuwa ni jambo lisilokubalika katika maisha yetu ya kila siku,
tunawajibika kulishughulikia kwa nguvu zote kila mahali na katika ngazi zote”.
Kwa mujibu
wa Taasisi ya UN-WOMEN zaidi ya asilimia 70 ya wanawake
katika baadhi ya nchi ni wahanga wa
ukatili au ukatili wa ngono katika maisha yao. Na katika nchi kama vile
Australia, Canada, Israel, Afrika ya Kusini na Marekani asilimia kati ya 40 na
70 vifo vya wanawake vinasababishwa na
masuala ya mapenzi.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa UN-WOMEN Bi. Michelle Bachelet amewaeleza
wajumbe wa Kamisheni hiyo kwamba, dunia
haiwezi tena kuendelea kuhimili gharama
za vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
Akaongeza
kwamba ni wakati muafaka na wa haraka
kwa serikali kuchukua hatua dhidi ya vitendo hivi ambayo anasema vinaendelea
kulalamikiwa katika jamii
Mwenyekiti wa CSW Balozi Marjon Kamara ambaye ni Balozi wa Liberia yeyé amesema katika wiki mbili za mkutano huo
wajumbe watajadiliana na kubadilishana mawazo kuhusu mbinu mbadala na
zinazotekelezeka za kuzuia ukatili dhidi ya wanawake na watoto wa wakike,
mbinu ambazo kweli zitaweza kuleta matokeo.
Pamoja
na Ujumbe wa Tanzania kushiriki kikamilifu katika mikutano na mijadala mbalimbali ambayo imo
ndani ya ratiba kuu ya CSW.
Tanzania nayo itakuwa na mijadala yake miwili ( side Events), kwa
lengo la kuonyesha uzoefu wa Tanzania katika kukabiliana na ukatili dhidi ya wanawake na watoto wa kike
Mjadala
wa kwanza umeandaliwa na washiriki
kutoka Tanzania Visiwani, mada yake
itahusu: Vunja ukimya, unga mkono juhudi
za sekta mtambuka katika kuzuia na
kukabiliana na unyanyasaji dhidi ya wanawake;
uzoefu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; mfano wa Zanzibar.
Na
mjadala wa pili umeandaliwa na Chama cha Majaji Tanzania,
utajadili kuhusu: Ukomeshaji wa matumizi
mabaya ya mamlaka kwa madhumuni ya
kudhalilisha kingono ( sextortion);
Uzoefu wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania.
No comments:
Post a Comment