ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, March 5, 2013

'Wahuni' wafyeka ekari 25 za mahindi

Bwana shamba wa shamba la Efatha lililopo Sumbawanga, Simon Jacob, akionyesha mahindi yaliyofyekwa na watu wasiojulikana na kusababisha hasara ya mamilioni ya fedha.

Picha na Mpiga picha Wetu
Watu wasiojulikana, wamevamia na kufyeka ekari 25 za mahindi katika shamba linalomilikiwa na Kanisa la Efatha la Sumbawanga. Tukio hilo lilitokea wiki iliyopita na eneo lililofyekwa ni sehemu ya ekari 96 za shamba hilo. Akizungumzia tukio hilo, Meneja wa shamba hilo, Peter Kibona, alisema liligunduliwa na vijana wake walipokuwa wanakwenda shambani kwao.

“Walipofika katika eneo hilo, vijana walishangaa kukuta mahindi yakiwa yamefyekwa katika eneo kubwa, kwa kweli inasikitisha sana,” alisema Kibona.
Meneja huyo alisema waliofanya kitendo hicho, wameteketeza kiasi kikubwa na chakula ambacho kingesaidia jamii katika siku zijazo.

“Ekari moja inazalisha gunia 20 na kwa hesabu hizo, ekari 25 tungepata magunia 500 ya mahindi,” alisema Kibona.

Alisema tayari uongozi wa shamba hilo umetoa taarifa za tukio hilo.
Meneja huyo wa shamba, alisema kumekuwa na mfululizo wa matukio katika shamba hilo linalomiliki kihalali na kanisa.

“Wananchi waliwahi kuchoma matrekta mapya mawili yanayomilikiwa na Efatha jambo ambalo ni hasara kwao,” alisema.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Rukwa, Jacob Mwaruanda, alisema polisi wana taarifa za tukio hilo na kwamba tayari wameanza kufanya upelelezi ili kujua wahusika na lengo lao.

5 comments:

Anonymous said...

Kwenye kichwa cha habari mwandishi amewaita "WAHUNI" Kwenye habari kamili amewaita "WATU WASIOJULIKANA" Kwahiho kama mtu hajulikani anakuwa muhuni? Na kama hawajulikani mwandishi amejuaje kama wao ni wahuni. Samahani nimeuliza kwasababu napenda kuendelea kujifunza lugha yangu ya Kiswahili.

Anonymous said...

Mmhh, unyofu wa lugha au kupinga pinda kwa lugha siyo tatizo. Ujumbe umeupa mh. Nony hapo juu pa march 5 4:06pm. Kwa kanisa la Efatha, je mmejiuliza na kupata jibu? Kwa uelewa wangu, shamba hilo mlilipata bila ridhaa ya wananchi, bali mlijipendekeza kwa serikali mkimwaga fedha nyingi ambazo ziliingia ktk mikono ya wachache.

Ushauri wangu ni huu ! "TAFUTENI KWA BIDII KUWA NA AMANI NA WATU WOTE." Waebrania 12:14.
Kanisa kaeni na wananchi wanaozunguka eneo hili sababu Mungu asipolinda, mlindao mwafanya bure.

Anonymous said...

Nashukuru sana mtoa maoni wa pili. Mini ndiye mtoa maoni wa kwanza kabisa hapo juu. Sihusiani kabisa na kanisa lililotajwa na wala silifahamu. Mimi nasali msikitini. Nilichotaka kufahamu ni kuwa wale wote wasiojulikana na mwandishi ni wahuni? Tatizo langu siyo kanisa wala shamba, bali ni ethics of journalism. Kama mimi na wewe hatujulikani kwa huyu mwandishi, maana yake sisi ni wahuni.

Anonymous said...

mtoa maoni wa pili nafikiri unafahamu kuwa nchi inaongozwa na sharia na katiba, na siyo mashairi ya vitabu vya dini. Kama shamba lilitolewa kimakosa, sharia si zipo? tukisema kila mddhurumiwa aanze kufyeka shamba la mdhurumu, tutakuwa kama jirani zetu Kenya na tutakaoumia ni sisi sote na vizazi vyetu. Every civil society uses the rule of law to settle disputes and not violence.

Anonymous said...

Mimi kwa mtazamo wangu nafiki wahuni ni wanaume waojisaidia haja ndogo wakiwa wamechuchumaa, au wanawake wanaifanya hivyo wakiwa wamesimama. Nadhani hao ndio mwandishi anaotaja kufyeka shamba la mahindi.