Sam Mapenzi wa Skylight Band akifanya vitu vyake kwa Stage kwenye show zao za Kila Ijumaa katika Uwanja wao wa Nyumbani Thai Village Masaki jijini Dar. Wakazi wa Mwanza kaeni mkao wa Kula SKYLIGHT BAND itatua huko mwisho wa mwezi kusheherekea Pasaka na mashabiki wake.
You a bad girl and your friends bad too, oh.. We got the swag sauce, she drippin' swagu...You a bad girl and your friends bad too, oh We got the swag sauce, she drippin' swagu...!!! Sam Mapenzi katika Collabo na Aneth Kushaba a.k.a 47 wakiimba wimbo wa 'PARTY' wa Beyonce aliomshirikisha Andre 3000.
Warembo wakichizika na Skylight Band.
Mashabiki wa SKYLIGHT BAND mdogo mdogo wakijimwaga stejini baada ya kupandishwa mzuka na wasanii wa Band hiyo.
Aneth Kushaba AK 47 akiwapa raha mashabiki wa Skylight Band kwenye kioata cha Thai Village Masaki.
kwa picha zaidi bofya
Wadau wakiendelea kuburudika na vinywaji huku Skylight Band ikiendelea kutumbuiza.
Mdau Alex All the way from Bagamoyo alikuja kuona Live Show ya Skylight Band baada ya kuona matukio ya Band hiyo kwenye Mtandao wa Mo Blog. Shukrani za pekee mdau Much respect..!!
Mashabiki wa Skylight Band wakiendelea kula bata kwa raha zao.
Sam Mapenzi akitunzwa na Pedeshee wa kike manoti kibao, baada ya kukunwa na uimbaji wa kijana huyo.
Sebene limekolea.....Mashabiki wa Skylight Band wakitweta jasho kwa kucheza. Njoo na wewe Ijumaa ijayo uburudike na kupunguza Stress.
Joniko Flower akiongoza wenzake Sam Mapenzi na Sony Masamba kutoa burudani kwa mashabiki wa Skylight Band.
Hiyo inaitwa abiaria chunga mzigo wako.....
Kila mtu bwana anashida zake, ziache zako kwenu njoo kati tucheze....Carolina usiondoke mama mziki bado wee...Carolina usiniache nyuma nitacheza nawe.....Si Mwingine ni Mary Lukas uzao wa BSS akishusha mistari nyimbo ya Carolina inayobamba katika TV na Radio Stations nchini kote.
Mashabiki wa Skylight Band wanapokolewa na utamu wa nyimbo ya Carolina inakuwa hivi.
Mary Lukas na Aneth Kushaba AK47 wakionyesha umahiri wao katika kunengua jukwaani.
Kikosi kazi cha Skylight Band kikishambulia jukwaa.
Mpiga Drum wa Skylight Band akiwajibika.
Mashabiki wa Skylight Band wakimwaga radhi na mduara uliokuwa ukiporomoshwa na Mary Lukas na hivi ndivyo inavyokuwa.
Unaambiwa mwanamke nyonga hasa pale unapojua kuizungusha kama huyu dada hapo pichani. Chezea Mduara wewee ni Balaaa...asiyekuwepo na lake halipo.
Bamutu na pesa zao wakishow love....mbele ya Camera ya Mo Blog.
Twin Sisters...!
Crew ya Maujanja Supplier wanaompendezesha mwimbaji wa Skylight Band Sam Mapenzi nayo ilikuwepo.
Msanii wa Bongo Flava Ngwair ambaye hakosi Show za Skylight Band akishow love na camera yetu.
Shekha akishika tumbo la Mama Kijacho.
Mashabiki nambari 1 wa Skylight Band. Mdau akionyesha ishara ya kuikubali Band hiyo kutoka moyoni kabisa.
Mboni Masimba wa 'The Mboni Show' akishow love na mashabiki wake Skylight Band.
Warembo waukweli ndani ya Skylight Band.
Kichuna wa ukweli....na mdau King Kif.
King Kif akishow love na Wala bata wa mujini. Ukienda Maisha wapo....Kila sehemu wapo, nani anabisha...??
Mdau Alois Ngonyani na Mary Lukas wa Skylight Band wakishow love.
Q Chilla na Sound Engineer wa Skylight Band.
Bata liliishia hapo tukutane tena Ijumaa ijayo pale pale Thai Village Masaki.
No comments:
Post a Comment