ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, March 6, 2013

WATANZANIA DMV TUWE MACHO .

Ndugu zangu Watanzania kunawizi mpya  umeingia DMV na kwengineko ndio maana ninaandika taarifa hii kuwatahadhari.

Siku ya Jumanne March 5, 2013 Mtanzania anaeishi maeneo ya Rockville  hapa Maryland  ambae hakutaka jina lake litajwe, alisema alipokua kazini alipokea simu kutoka kwa wanae wakisema kuna mtu anawapigia simu akiwaambia wamemteka baba yao na wamemuekea bastola kitwani na kuendelea kusema kwamba wanachohitaji ni pesa ili waweze kumuachia wasipofanya hivyo watamlipua kichwa kwa risasi na kumuua.

Watoto waliposikia maneno yale waliogopa wasijue la kufanya na kumpa jamaa yule simu ya mama yao ambae kwa wakati ule alikuwepo kazini, wakati wanafafanya hivyo walipiga simu ya mkononi ya baba yao kuona kama itapokelewa mara baba yao akapokea simu wakamueleza kilichotokea na baba akawaambia wapige simu polisi.wawataarifu kichotokea na wamumpigie mama yao.

Wakati huo wale jamaa walimpigia mama yao wakamuambia tumemteka mume wako tumemuekea bastola kichwani tunachohitaji ni pesa usipotutumia pesa tutamlipua kichwa kwa risasi na hautamuona tena. Mama aliposikia maneno yale maswali mengi yasiyokua na majibu yalimuijia kichwani na hatimae akapata jibu la kuwaambia sasa hizi nina mgojwa tafadhali nipigieni baada ya dakika 15 tuongee zaidi na jinsi gani ya kuwapatia hiyo pesa.

Wakati anakata simu akampigia mume wake na kumuuliza kama yupo salama na kuulizwa kutekwa kwake na jinsi alivyopigiwa simu, mume wake akamuambia mimi nipo kazini salama sijui kinachoendelea watoto nao walinipigia simu tafadhali nenda nyumbani na waujulishe polisi.

Polisi walitaarifiwa nao bila ajizi walifika hapo nyumbani na ndipo walipowaeleza jambo hili ni wizi ulioingia watu hawa waaishachukua pesa kwa watu wengi na wala hawaishi maeneo hayo wanachokifanya ni kusema kama walivyofanya ili kuwatisha familia na wewe kuwatumia pesa kupitia western Union.

Kwa hiyo Watanzania wenzangu habari ndio hiyo nimeona tushee kusudi simu kama hii itakapopigwa kwako au kwenye familia yako ujue ni kitu gani cha kufanya Asante.

2 comments:

Anonymous said...

Asante sana mtoa mada kwa muda wako na dhamira yako ya kutuelimisha. Asante DJ Luke pia. Wizi wa aina hiyo unafanywa sana na kikundi cha genge cha Mala Salvatrucha (MS-13) and most victims are people from Hispanic community (Unaweza ku-google utawaona) Mara nyingi wakisha kutisha watakwambia utume pesa Florida au El-Salvador. Ukipokea simu kama hiyo usipanic wala usiwatukane. Just be calm and politely disengage in conversation and hang up the phone then report to police immediately.

Anonymous said...

Hapo kunanitatiza kidogo,kama umepokea simu ya hao maharamia kuwa wamemuataki mmoja ya familia yako ,na ukampigia simu yuko salama hawajamkidinapu,hao watu wanakua hawajafanya hivyo sasa wizi wao huo uko wapi?mimi sijaelewa lakini kuwataarifu polisi ni muhimu,hebu nielewesheni since sioni kama inaogopesha.Asanteni.