ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, March 7, 2013

WAZAZI NA WADAU JIJINI WAKARIBISHWA KATIKA UFUNGUZI WA SHULE MPYA YA AWALI YA ONE PLANET SIKU YA JUMAMOSI MACHI 9 2013.

Baadhi ya vifaa vya michezo mbalimbali katika shule ya kisasa ya One Planet Pre School and Day Care Centre.
Mkurugenzi wa One Planet Pre and Nursery School Bi. Elizabeth Mahiga akizungumza na vyombo vya habari Dar es Salaam leo kuhusu shule hiyo, ambapo amesema ni ya kawaida kwa ajili ya watoto ili kuwakuza watoto waweze kuwa tayari katika fani zote kwa kutumia michezo mbalimbali, ngoma na sanaa ya uchoraji ili kuamsha ufahamu wao.
Amesema shuleni hapo wanapokea watoto wa aina zote bila kubagua jinsia, ulemavu wa viungo, rangi, dini, lugha na kuwa mtoto anatoka katika familia gani.
Aidha Bi. Mahiga amewataka watanzania kutohofia mazingira ya shule na kuweka wazi kuwa gharama zao ni nafuu ni kuanzia shilingi 10,000/= kwa siku na mtoto anashinda katika mazingira salama akiwa na walezi wake na kuongeza kuwa katika shule hiyo hawaandai chakula kwa ajili ya watoto kwa kuwa wengine wana uzio (Allergy) na baadhi ya vyakula hivyo ni vyema wazazi wakamuandalia nyumbani akaja kula akiwa shule.
Picha juu na chini ni Sehemu maalum ya One Planet Pre School and Day Care Centre yenye bustani iliyonawiri ambayo imetengwa kwa ajili ya watoto kufanya michezo mbalimbali kwenye hali ya usalama.
Picha juu na chini ni Muonekano wa ndani wa baadhi ya madarasa ya watoto katika shule hiyo.
Baadhi ya walezi na walimu wa shule hiyo wakiwaongoza watoto wakati wa kipindi cha Michezo.
Baadhi ya watoto wanaosoma shuleni hapo wakicheza michezo mbalimbali.
Muonekano wa jengo la shule hiyo lenye madarasa sita likiwemo darasa la Ngoma na Muziki kwa watoto.
Shule mpya ya kisasa kwa ajili ya watoto wenye umri wa miezi sita mpaka miaka mitano ya One Planet Pre and Nursery School inawakaribisha wazazi, wadau na wapenda maendeleo katika sekta ya elimu katika siku ya ufunguzi wa shule “FUN DAY”.

Ufunguzi huo utafanyika Jumamosi Machi 9 mwaka huu kuanzia Saa 3 asubuhi mpaka Saa kumi katika viwanja vya shule hiyo iliyopo Msasani Mwisho, 230 Uganda Avenue jijini Dar es Salaam bila kiingilio.

Siku hiyo itatoa fursa za kukutana na kubadilishana mawazo na walimu wa watoto haea, michezo mbali mbali ya watoto na pia, wazazi kukutana na kufahamiana (Networking)ili kujenga misingi mizuri kwa ajili ya ya manufaa ya maendeleo ya mwanao kimasomo.

Lugha inayotumika kufundishia shuleni hapo ni Kiingereza na Kifaransa.

No comments: