Kikosi cha timu ya Azam kiliondoka nchini jana jioni kuelekea Morocco kujiandaa kwa mechi yao ya marudiano ya raundi ya pili ya michuano ya Kombe la Shirikisho dhidi ya wenyeji AS FAR Rabat huku kocha wa wawakilishi hao pekee wa Tanzania katika mashindano ya Afrika, Stewart Hall akisema kwamba watatumia mbinu ya 'kupaki basi' ili kujilinda zaidi na kushambulia wapinzani wao kwa kustukiza.
Mechi hiyo ya marudiano itachezwa Jumapili (Mei 5) na Azam ambao walishikiliwa kwa sare ya 0-0 katika mechi yao ya kwanza kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, watahitaji walau sare yoyote ya mabao ili kutimiza ndoto ya kufuzu kwa hatua ya makundi ya michuano hiyo.
Akizungumza na NIPASHE jijini Dar es Salaam jana asubuhi, Hall alisema kuwa wanajiandaa kujilinda zaidi kwa nia ya kudhibiti mashambulizi ya maana langoni kwao lakini wakati huo huo, wakihakikisha kuwa wanalishambulia lango la wenyeji kwa kasi kila mara watakapopata mpira, hasa wakitumia pasi ndefu zitakazowafikisha mapema kwenye eneo la hatari la Rabat.
Kocha huyo alisema kuwa wameshawashika kutumia mbinu hiyo baada ya kubaini wakati wa mechi yao ya kwanza kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kuwa wapinzani wao husumbuliwa na pasi ndefu na mashambulizi ya kustukiza.
Kocha huyo ambaye aliwahi pia kuifundisha klabu ya Sofapaka ya Kenya, alisema kuwa kwa mbinu hiyo, wana uhakika wa kuwaondoa Wamorocco na kufuzu kwa hatua inayofuata, licha ya kwamba hii ni mara ya kwanza kwa klabu yao kushiriki mashindano yanayoandaliwa na Shirikisho la Soka la Afrika (CAF).
"Tunakwenda kupambana na si kukamilisha ratiba. Tunajua mechi itakuwa ngumu kwa pande zote huku wageni tukipewa nafasi ndogo ya kushinda... sasa tunafahamiana na hivyo kila upande utacheza kwa tahadhari kubwa," alisema Hall.
Kocha msaidizi wa Azam, Kally Ongalla, ambaye alikuwa kwenye kundi la kwanza la viongozi waliotangulia Morocco, alisema hali ya hewa waliyoikuta Morocco ni ya baridi linalofanana na Arusha, na kwamba hadhani kama itawasumbua wachezaji wao ambao wamezoea zaidi joto la Dar es Salaam.
Kikosi cha Azam kinatarajiwa kutua nchini Morocco leo mchana baada ya jana usiku kulala Dubai.
Azam ndiyo wawakilishi pekee wa Tanzania waliobaki kwenye mashindano ya kimataifa baada ya Simba kutolewa katika raundi ya awali ya Ligi ya Klabu Bingwa Afrika kutokana na kipigo cha jumla ya mabao 5-0 walichokipata kutoka kwa Recreativo de Libolo ya Angola. Jamhuri ya Pemba pia iliaga mapema huku Azam iking'ara kwa kuzing'oa Al Nasr ya Sudan Kusini na Barrack YC ya Liberia.

CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment