Kwa hatua hiyo, imesema pia itaendelea kuwa makini na kutoruhusu ujenzi holela hasa wa maghorofa.
Hayo yalisemwa juzi na Kaimu Mkurugenzi wa CDA, Pascas Muragili katika mkutano wake na waandishi wa habari.
Jengo lililovunjwa lipo katika barabara ya 11 mjini hapa, ambapo mhusika ametambuliwa kwa jina moja la Massawe.
Alibainisha kuwa mmiliki wa jengo hilo amekimbilia mahakamani kufungua kesi kupinga kuvunjwa kwa jengo lake, akidai kuonewa.
Alisema hakukuwa na kibali cha ujenzi huo, kwani nyumba hiyo ilikuwa ya kawaida na mmiliki aliamua kuongeza ghorofa juu.
Akizungumzia suala la wapangaji wa nyumba za CDA zilizopo Kikuyu kugoma kuondoka kupisha ukarabati, alisema kwa kuwa suala hilo liko mahakamani watasuburi mahakama iamue.
Alisema mwaka 2008, CDA ilipandisha kodi katika nyumba hizo ambapo walikuwa wakilipa Sh 22,000 kwa vyumba vitatu, Sh 18,000 vyumba viwili na nafasi kubwa na Sh 15,000 kwa vyumba viwili na nafasi ndogo.
Alisema walipendekeza kupandisha kodi iwe Sh 55,000 kwa vyumba vitatu ndipo wapangaji wakasema walikuwa wakionewa kodi kubwa hawalipi na ilikuwa imekwenda kinyume na makubaliano ya siku za nyuma.
Aliongeza kuwa wapangaji hao walikwenda Baraza la Ardhi la Wilaya ambalo liliamua walipe kodi mpya ya Sh 55,000 lakini hawakukubaliana na uamuzi huo na badala yake kukata rufaa Mahakama Kuu kupinga uamuzi wa Baraza.
Katika uamuzi Mahakama Kuu iliridhika kwani kulikuwa na makubaliano kati ya wapangaji na CDA na mahakama ilisema mamlaka hiyo hairuhusiwi kupandisha kodi hadi itakapofanyika ukarabati nyumba zake.
Pia baada ya matengenezo, kodi mpya ya CDA lazima iendane na soko na kutokana na makubaliano hayo ya mahakama, wakatafuta mkandarasi ili kufanyia matengenezo makubwa katika nyumba hizo ikiwemo kurekebisha mfumo wa vyoo, lakini wapangaji hao walikataa na kukimbilia tena mahakamani.
Alisema kuwa kuna jumla ya familia 174 katika nyumba hizo na mafundi hawawezi kufanya lolote mpaka wapangaji hao wahame kutokana pia na sababu za kiafya.
Aliongeza kwamba kwa kuwa wapangaji hao wamekimbilia mahakamani na Mahakama Kuu kuamuru wasiondolewe mpaka kesi ya msingi itakaposikilizwa, wanasubiri uamuzi huo ili waone nini cha kufanya.
Pia alibainisha kuwa wafanyakazi wanne kati ya 14 ambao ni wapangaji katika nyumba hizo tayari wameondoka na waliobaki wako mbioni kuhama.
Sifa Lubasi,Habarileo
No comments:
Post a Comment