
Young Africans Sports Club.
Official Young Africans Sports Club VPL CHAMPIONS 2012/2013.

Yanga wametwaa ubingwa baada ya kusaidiwa na matokeo ya mchezo kati ya timu iliyokuwa inagombania ubingwa na Yanga Azam Fc kutoka sare ya 1-1 na Coastal Union katika mchezo uliopigwa huko Mkwakwani Tanga .
Yanga wanatwaa ubingwa kwa sababu matokeo ya sare yameifanya Azam Fc kufikisha pointi 48 huku ikiwa imesalia michezo miwili kabla ya ligi kumalizika hivyo kushindwa kuifikia Yanga yenye pointi 56, ambapo hata Azam ikishinda michezo miwili iliyosalia itafikisha pointi 54 pekee.
Yanga imebakiza michezo miwili ambayo itacheza dhidi ya coastal Union na mahasimu wao wa jadi Simba Sports Club kwenye siku ya mwisho ya ligi .
No comments:
Post a Comment