Maua akiwa kwenye darasa la kiswahili lililoendela leo Jumamosi April 6, 2013 College Park, Maryland
Wanafunzi wakiwa na darasa la kiswahili linaloendelea kila Jumamosi hapa DMV chini ya uongozi wa Jumuiya.
Viongozi, Wajumbe na wazazi wakipata picha ya pamoja huku wakiwasubiria watoto wamalize darasa lao la kiswahili.
Wanafunzi wakiendelea na darasa lao DMV
Wanafunzi wakiwa darasani
Mwalimu wa darasa la kiswahili, dada Asha Nyang'anyi akiendelea kuwanoa watoto kwenye darasa la kiswahili, DMV
Uongozi wa DMV pamoja na mjumbe, mama Kimolo ( watatu toka shoto) katika picha ya pamoja wakifuatilia maendeleo ya wanafunzi.
Wanafunzi wakifuatilia somo la kiswahili na wengine wakitupia macho kwenye kamera ya Vijimambo.
Mwalimu, dada Benadeta akimfuatilia mwanafunzi wake.
Kiswahili, kiswahili, mwanafunzi akitafakali jambo kwenye darasa lake la kiswahili.
kwa picha zaidi bofya read more
12 comments:
You guys are for real. Nawapenda sana watz wa DMV. Mungu awabariki sana na muendelee na moyo huo mlionao. Pale mlipopunguza Mungu atawazidishia mara dufu.
Mwalimu dada Bernadeta naomba namba yako ili uwasaidia watoto wangu kujua Kiswahili.
kwa roho safi tu nauliza swali mwalimu ana shahada za ualimu? kama hajafunzwa kufundisha watoto naomba muwaachie waliosomea kazi zao wazifanye ili wawapatie watoto mafunzo yanayostahili maana kuongea kiswahili haina maana wewe ni mwalimu samahani kama nimemkwaza mtu yoyote
msemaji hapo juu unaonaje ukapeleka mapendekezo yako ya msingi kwa uongozi wa darasa hilo kistaharabu ili ufanyiwe kazi?
Wewe anonymous wa april 6, 2013 at 9;48pm - Hao wenye shahada za ualimu mbona hatujawaona hapa DMV? Mimi nimeishi hapa for 20yrs na hatujawahi kuwasikia hao unaowasema wakijitangaza kufundisha kiswahili kwenye community yetu FOR FREE. Hatutaki NEGATIVITY WE NEED SUPPORT AND POSITIVE MIND, na kama unawajua please wajulishe kuwa madarasa yapo na tunawakaribisha kujuuika nasi. Anybosy can teach swahili kuna guidance za teach swahili yourself, teach kids swahili online you can use to teach anybody who is not a swahili speaker and you do not need a shahada ya ualimu! THIS IS A COMMUNITY SERVICE KWA JUMUIYA YETU TUNAJITOLEA KUWAFUNDISHA WATOTO FOR FREE. LETS BE POSITIVE AND THIS IS THE ONLY WAY WE CAN CHANGE DMV!!!! ASANTENI MNAOTUPA MOYO.
MWALIMU WA KISWAHILI DMV
Asanteni sana,wadada mliojitolea kufundisha. Mungu atawabariki. Tusonge mbele na msivunjike moyo na changamoto za hapa na pale. Nawashukuru sanasana kufundisha wanangu,na ninaona mabadiliko makubwa kwa uelewo wao ktk kiswahili. Mngeweza kudai malipo lakini la hasha ni buree!!! Je!ni wangapi watafanya hili? Tuwe wakweli wa nafsi kabsa! Mimi nitawaombea ktk sala zangu. Ahsante!
Kwa maoni yangu, wakati umefika waalimu na wanafunzi wakaachwa waendelee na shughuli ya kufundisha na kujifunza. Hili darasa lisifanywe kama tukio la kisiasa. Keep the cameras away from the classroom because their unbroken presence in the classroom can only serve as a distraction. Wasio waalimu na wasio wanafunzi pia should stay away from the classrom. PERIOD.
Dada Asha,Flora Mkande,Lucia na Bernadeta;Kwanza mimi binafsi nawashukuruni sana kwa moyo huu wa kuisaidia Community ktk kufundisha lugha yetu tukufu ya kiswahili,pili endeleeni na kazi na juhudi nzuri za kuwafundisha watoto wetu,kwa kweli wanangu wameshahudhuria madarasa mawili tu na sasa wanaanza kukichapa kiswahili murua kama kula ugali na mlenda vile(unajua tonge linavyokuwa laini)ndio maana yake. Siku zote penye mazuri kutakuwa na wachache ambao watajaribu kuwavunja moyo.USHAURI WANGU NI HUU: Viongozi wetu wa jumuiya na walimu wetu wa kujitolea endeleeni na juhudi zenu na sisi(mimi)wazazi tupo pamoja bega na bega na nyie kuwasaidia. IDUMU LUGHA YETU YA TUKUFU YA KISWAHILI
Hili darasa halina lengo la ku-produce swahili linguists bali kuwasaidia wasioongea kiswahili kupata basic communication skills za kiswahili. Hivyo mwalimu wa kiswahili kwa darasa hili si lazima awe na shahada ya kiswahili ingawa kama atakuwa nayo ni vizuri zaidi. Kumbuka mama wa kichaga, kinyakyusa, kihaya au wa kabila jingine lolote, anayemfundisha mwanae kichaga, kinyakyusa, n.k. pia hana shahada ya lugha hiyo, lakini huweza kutimiza lengo kale bila matatizo.
Nisichokubaliana nacho kwenye hili darasa ni kuruhusu distractions zinazosababishwa na cameras darasani. Can someone please tell me why do we need these cameras in the classroom? Hili sio jukwaa la kisiasa.
Please keep the cameras away from the classroom. Na wasio waalimu au wanafunzi nao pia should stay away from the classroom. It's time we let teachers do the teaching and the students do the learning free of any undue distractions!!!
Dj Luke endelea kutuletea picha za madarasa,na wazazi wanaotaka kutembelea ruksa,hata shule za hapa esp. Montgomery County,i can speak of my own,wakati wowote ukitaka kutembelea darasa ruksa. Access kwa mwanao ni right ya mzazi,period. We unaesema "nobody" asiwepo says who. Peleka maoni ktk uongozi then waweke taratibu zilizowazi kama watakubaliana na wewe. Hayo ni maoni yako binafsi sio sheria.
Kama mdau anaelalama kwa wasio waalimu,wazazi wanasubiria watoto wao,kuna wengine wanakuwepo darasa la vichekechea sababu mwalimu mojapeke yake sio rahisi,labda uongozi ueleze kuwepo na wasaidizi au la,na kama nawe ni mzazi,siku moja nenda kwa darasa la vichekechea ukasaidie. Kupeleka watoto restroom 2-4yrs old kama 15 kwa wakati moja. See how "fun" it is. I have been a volunteer with Montgomery county public schools,there are 2 adults all the time in pre-K classes. Mdau unaelalama nina wasiwasi unapata wapi facts zako au ni personal beefs???!!!
Mtanzani huna jema ,viongozi wa jumuia wanajitahidi, lakini malalamiko mengi,DJ LUKA,anajitahidi kuwaonyesha jinsi maendeleo ya jumuiya yetu ,bado mnaona ni vibaya,shughuli yeyote lazima ifuatiliwe kuhakikisha mambo yanakwenda vizuri wote hao ni viongozi wa jumuiya ,wajumbe wa bodi lazima wafuatilie kama yalivyokuwa makubaliano yao ,sasa wewe unasema kamera zikae mbali,umefanya nini ktk kusaidia jumuiya yetu kimaendeleo,kaka Luka hongera kwa kazi nzuri ya taarifa,viongozi NA WAJUMBE WA BODI wa JUMUIA HONGERENI SANA KWA KAZI NZURI MUNGU AWABARIKI
Post a Comment